Ukraine

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Україна
Ukrayina

Ukraine
Bendera ya Ukraine Nembo ya Ukraine
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: Ще не вмерла України
Shche ne vmerla Ukrajiny]]
"Ukraine's glory has not perished"
Lokeshen ya Ukraine
Mji mkuu Kiev (Kyiv)
50°27′ N 30°30′ E
Mji mkubwa nchini Kiev
Lugha rasmi Kiukraine
Serikali Demokrasia
Petro Poroshenko
Volodymyr Hroysman
Uhuru
ilitangazwa
Kura ya maoni ya wananchi
ilikubaliwa
24 Agosti 1991
1 Desemba 1991
25 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
603,700 km² (ya 44)
7%
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
44,291,413 (ya 32)
48,457,102
73.8/km² (ya 115)
Fedha Hryvnia ya Ukraine (UAH)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD .ua
Kodi ya simu +380

-


Ramani ya Ukraine

Ukraine (Україна, Ukraina) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki. Imepakana na Urusi, Belarus, Poland, Slovakia, Hungaria, Romania na Moldova.

Kuna pwani ya Bahari Nyeusi na ghuba ya Azov.

Mji mkuu ni Kiev (Kyiv).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kwa muda mrefu Ukraine ilikuwa sehemu ya Dola la Urusi.

Miaka 1918 - 1921 baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na ya kuporomoka kwa Dola la Urusi nchi ilikuwa na kipindi kifupi cha uhuru na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Miaka 1922 - 1991 Ukraine ilikuwa jamhuri mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti.

Hatimaye ilijipatia tena uhuru wake, ingawa Russia haijaridhika wala kukubali mipaka. Hivyo mwaka 2014 ilivamia rasi ya Krimea na maeneo mengine ya mashariki. Hadi leo hali ni ya vita.

Lugha[hariri | hariri chanzo]

Kwa muda mrefu Ukraine ilitawaliwa na Urusi na Kirusi kilikuwa lugha ya utawala hali halisi.

Tangu uhuru serikali imeendesha sera ya kujenga lugha ya taifa, pamoja na kujali lugha nyingine 18 za kieneo.

Hivyo Kiukraine (українська мова "ukrajin's'ka mova") ni lugha rasmi, lakini angalau nusu ya wakazi hutumia Kirusi.

Kiukraine ni lugha ya Kislavoni karibu sana na Kirusi.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Sensa ya mwaka 2001 ilionyesha ya kwamba 77.8% za wakazi hujiita "Waukraine". Waliojiita Warusi walikuwa 17.3%. Vikundi vingi vingine kama Wabelarus, Wamoldova, Watartari, Wabulgaria, Wapoland, Wayahudi na wengine walikuwa kila kimoja chini ya 1%.

Baada ya ukomunisti kupiga vita dini kwa njia zote na kwa miaka mingi, siku hizi wakazi wengi hawana dini yoyote.

Walionayo ni hasa Wakristo wa Kanisa la Kiorthodoksi la Russia, lakini Waorthodoksi wengine wamejitenga na kuanzisha Kanisa la Kiorthodoksi la Ukraina.

Pia kuwa waamini wengiwengi wa Kanisa Katoliki, hasa wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraina linalofuata mapokeo ya Kigiriki kama Waorthodoksi, lakini pia wa Kanisa la Kilatini.

Pamoja na hayo, idadi ya wakazi inazidi kupungua haraka.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ukraine kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.