Mapatano ya Budapest ya 1994

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mapatano ya Budapest ya 1994 (Kiing. Budapest Memorandum on Security Assurances) ni makubaliano kati ya Urusi, Ufalme wa Maungano na Marekani kuhusu Ukraine, Belarus na Kazakhstan.

Nchi hizo tatu zilizokuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi mwaka 1991 zilikuwa tayari kuachana na silaha za nyuklia ambazo ziliwahi kurithi wakati wa uhuru na kuzikabidhi kwa Urusi. Hapo washiriki watatu wa Mapatano ya Budapest waliahidi kwa kila nchi kuheshimu uhuru na mipake yake na kutoitisha au kutumia silaha dhidi yake kamwe.

Urusi, Ufalme wa Maungano na Marekani ziliahidi katika mapatano hayo

  1. kuheshimu uhuru na mamlaka na mipaka ya Ukraini, Belarus na Kazakhstan iliyopo wakati wa 1994[1]
  2. kutotumia matishio au nguvu dhidi ya umoja au uhuru wa Ukraini, Belarus na Kazakhstan, na kwamba hawatatumia kamwe silaha zao dhidi ya nchi hizo, isipokuwa kwa kujitetea[2].
  3. kamwe kutumia mashurutisho ya kiuchumi dhidi ya Ukraini, Belarus na Kazakhstan ili kuzuia nchi hizo kutekeleza haki za mamlaka huru (sovereignty) na hivyo kujipatia faida zozote.[3]
  4. ikiwa Ukraini, Belarus na Kazakhstan zinashambuliwa, nchi tatu za mapatano zitatafuta mara moja hatua kupitia Baraza ya Usalama ya UM.[4]

Mapatano yalitolewa kwa nakala kwa kila nchi kwa lugha za Kiukraine, Kirusi, Kiingereza na Kifaransa na kutiwa sahihi na kila nchi husika mjini Budapest tarehe 5 Desemba 1994.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. The Russian Federation, the United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland, and the United States of America reaffirm their commitment to Ukraine ... respect the independence and sovereignty and the existing borders of Ukraine.
  2. The Russian Federation, the United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland, and the United States of America reaffirm their obligation to refrain from the threat or use of force against the territorial integrity or political independence of Ukraine, and that none of their weapons will ever be used against Ukraine except in self-defense or otherwise in accordance with the Charter of the United Nations
  3. The Russian Federation, the United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland, and the United States of America reaffirm their commitment to refrain from economic coercion designed to subordinate to their own interest the exercise by Ukraine of the rights inherent to its sovereignty and thus to secure advantages of any kind.
  4. The Russian Federation, the United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland, and the United States of America reaffirm their commitment to seek immediate United Nations Security Council action to provide assistance to Ukraine ... if Ukraine should become a victim of an act of agression.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mapatano ya Budapest ya 1994 kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.