Belarus
| |||||
| Kaulimbiu ya taifa: | |||||
| Wimbo wa taifa: Belarusian: Мы, беларусы (Mi Belarusi) ("Sisi Wabelarus") | |||||
| Mji mkuu | Minsk | ||||
| Mji mkubwa nchini | Minsk | ||||
| Lugha rasmi | Kibelarus, Kirusi | ||||
| Serikali | Jamhuri Alexander Lukashenko Roman Golovchenko | ||||
| Uhuru Ilitangazwa ilianzishwa ilikamilishwa |
27 Julai 1990 25 Agosti 1991 25 Desemba 1991 | ||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
207,600 km² (ya 84) kidogo sana (183 km²)[1] | ||||
| Idadi ya watu - 2025 kadirio - 2019 sensa - Msongamano wa watu |
9,109,280 (ya 98) 9,410,000 45.8/km² (ya 142) | ||||
| Fedha | Rubel ya Belarus (BYN) | ||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
FET (UTC+3) FET (UTC+3) | ||||
| Intaneti TLD | .by | ||||
| Kodi ya simu | +375
- | ||||

Belarus (kwa Kibelarus: Беларусь (Kisirili) au Byelarus (Kilatini); kwa Kirusi: Белоруссия) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki inayopakana na Urusi, Ukraini, Polandi, Lithuania na Latvia.
Mji mkuu ni Minsk na miji mingine ni pamoja na Brest, Hrodna, Homyel, Mahiylov na Vitsyebsk.
Historia
[hariri | hariri chanzo]


Belarus haikuwahi kuwa nchi ya pekee hadi karne ya 20. Maeneo yake yalikuwa chini ya himaya mbalimbali kama vile Polandi, Lithuania na Urusi. Katika karne za hivi karibuni, nchi imeteseka sana kutokana na Urusishaji.
Belarus ilikuwa jimbo la Umoja wa Kisovyeti tangu 1919/1922 hadi 1991. Mnamo 1932-1933 Belarusi ilikumbwa kidogo na njaa kubwa iliyoandaliwa na serikali ya kiimla ya Kisovyeti, na kupoteza mamia ya maelfu ya watu, wakati Ukraine ilipoteza mamilioni. Mnamo 1937, wasomi wote wa sayansi na wasomi wa Belarusi waliharibiwa na huduma maalum za Kisovyeti. Mnamo 1942, mwandishi mkuu wa Belarusi, Yanka Kupala, aliuawa. Mnamo 1950-1980, urithi wa usanifu wa Belarusi ulibomolewa.
Baada ya umoja huo wa majimbo 15 kusambaratika, Belarus ilijitangaza nchi huru. Mnamo 1991, nchi ilipata uhuru, lakini mnamo 1995, udikteta wa Alexander Lukashenko ulianza: katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, alibadilisha alama za watu kuwa zile za Kisovyeti zilizorudi na kutoka sera yake, watu wa Belarusi wako chini ya tishio la kutoweka.
Wakazi na utamaduni
[hariri | hariri chanzo]Wakazi walio wengi ni Wabelarus (84.9%) ambao wanaongea ama Kibelarus au Kirusi ambavyo vyote viwili ni lugha rasmi. Lugha hizi mbili zina asili moja. Takriban 7.5% za wakazi ni Warusi, 3.1% ni Wapolandi, 1.7% ni Waukraini. Hivyo kuna vikundi vidogo vinavyotumia lugha za pekee kama vile Kipolandi, Kiukraini, Kilatvia, Kilituanya na nyingine.
Walio wengi ni wafuasi wa Ukristo (91%), hasa katika Makanisa ya Kiorthodoksi (83.3%) na katika Kanisa Katoliki (6.7%).
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya mji wa Minsk Ilihifadhiwa 2 Novemba 2017 kwenye Wayback Machine.
| Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Belarus kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |