Jan Mayen
Mandhari
Jan Mayen ni kisiwa cha Norwei katika eneo ambapo Bahari ya Aktika na Atlantiki ya Kaskazini zinakutana. Eneo lake ni km² 373, urefu ni km 54 na upana km 2.5-15. Kisiwa kipo katikati ya Norwei, Isilandi na Greenland.
Hakuna wakazi wa kudumu isipokuwa wafanyakazi 14 wa vituo viwili vya serikali ya Norwei. Moja ni kituo cha redio kinachohudumia usafiri kwa ndege katika sehemu hii ya dunia. Nyingine ni kituo cha wataalamu wanaopima hali ya hewa.
Jan Mayen kilitangazwa kuwa sehemu ya Norwei 27 Februari 1930. Kiutawala kiko chini ya gavana wa Spitzbergen.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Satellite Radar image of Jan Mayen Ilihifadhiwa 31 Oktoba 2015 kwenye Wayback Machine.
- Photographs and information on Jan Mayen Ilihifadhiwa 31 Oktoba 2015 kwenye Wayback Machine.
- Jan Mayen crew Ilihifadhiwa 22 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
- LORAN-C mast Jan Mayen
Makala hii kuhusu maeneo ya Norwei bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jan Mayen kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |