Liturujia ya Ugiriki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mapokeo ya Kigiriki)
Undani wa Kanisa kuu la Utatu Mtakatifu, Chicago, Marekani.
Padri akiingia patakatifu akishika kitabu cha Injili.
Somo la Injili.
Litania ya wakatekumeni.
Padri akiingia patakatifu akibeba vipaji huku shemasi mdogo akishika chetezo.
Padri akisimama kwenye meza takatifu (altare).
Waamini wakijiandaa kupokea Ushirika mtakatifu.
Ugawaji wa Ushirika mtakatifu kwa waamini.
Askofu akifanya ishara ya msalaba kwa kitabu cha Injili juu ya kitambaa cha altare kiitwacho antimension.
Padri akiruhusu waamini kuondoka kwa msalaba wa baraka.

Liturujia ya Ugiriki, iliyoenea kutoka Konstantinopoli, sasa Istanbul (nchini Uturuki) ni liturujia ambayo lugha yake asili ni Kigiriki, lakini siku hizi inaadhimishwa katika lugha nyingine nyingi kukiwa na tofauti ndogondogo duniani kote.

Wanaoitumia hasa ni Waorthodoksi wote na baadhi ya Makanisa Katoliki ya Mashariki: hivyo ni ya pili kwa uenezi baada ya liturujia ya Roma.

Vitabu vyake vinaongoza Liturujia ya Kimungu (Ekaristi), Vipindi vya sala rasmi, Mafumbo matakatifu (Sakramenti) na sala, baraka na mazinguo mbalimbali, vilivyostawi katika Kanisa la Konstantinopoli.

Liturujia hiyo inahusika pia na namna maalumu za usanifu majengo, picha takatifu, muziki wa liturujia, mavazi na mapokeo zilizostawi vilevile karne hata karne kila ilikotumika.

Kwa kawaida mkusanyiko wa waamini huwa wamesimama muda wote wa ibada, na ukuta wa picha takatifu unaoitwa iconostasis unawatenganisha na patakatifu anapohudumia askofu au padri akisaidiwa na shemasi.

Ushiriki wa walei unajitokeza katika kusujudu mara nyingi na kuitikia sala na nyimbo.

Katika liturujia hiyo Biblia inatumika sana katika masomo na katika matini mengine vilevile.

Taratibu za saumu ni kali kuliko zile za Ukristo wa Magharibi na zinafuatwa katika vipindi vinne kwa mwaka: Kwaresima Kuu, Kwaresima ya Noeli, Mfungo wa Mitume na Mfungo wa Kulala kwa Bikira Maria. Pamoja na hayo, Jumatano na Ijumaa nyingi ni za kufunga chakula. Monasteri nyingi zina mfungo hata Jumatatu zote.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Liturujia hiyo ilianza kwa kufuata liturujia ya Siria, kwa kuwa kabla ya mwaka 381 Mashariki ya Kati ilikuwa chini ya Kanisa la Antiokia).

Mwaka huo Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli ulifanya mji huo kuwa na Patriarki wake, wa pili baada ya askofu wa Roma tu[1]. Hapo liturujia hiyo ilizidi kupata sura ya pekee kwa kuathiriwa hata za desturi za ikulu ya kaisari iliyokuwepo Konstantinopoli.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. First Council of Constantinople, Canon III

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Robert F. Taft, The Byzantine Rite. A Short History. Liturgical Press, Collegeville 1992, ISBN 0-8146-2163-5
  • Hugh Wybrew, The Orthodox Liturgy. The Development of the Eucharistic Liturgy in the Byzantine Rite, SPCK, London 1989, ISBN 0-281-04416-3
  • Hans-Joachim Schulz, Die byzantinische Liturgie : Glaubenszeugnis und Symbolgestalt, 3., völlig überarb. und aktualisierte Aufl. Paulinus, Trier 2000, ISBN 3-7902-1405-1
  • Robert A. Taft, A History of the Liturgy of St John Chrysostom, Pontificio Istituto Orientale, Roma 1978-2008 (6 volumes).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Ugiriki kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.