Nenda kwa yaliyomo

Mfungo wa Mitume

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya karne ya 13 ikiwaonyesha Mitume Petro na Paulo (Belozersk).
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki

Mfungo wa Mitume (pia: Mfungo wa Mitume Watakatifu, Mfungo wa Petro na Paulo, Mfungo wa Mt. Petro na hata Mfungo wa Rafik) [1] ni mfungo unaofanywa na Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki wa Mashariki.

Mfungo huo unaanza Jumatatu ya pili baada ya Pentekoste (siku baada ya Jumapili ya Watakatifu Wote) na kuendelea hadi sikukuu ya Mitume Petro na Paulo inayoadhimishwa tarehe Juni 29.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kisha kufurahia Ufufuko wa Yesu kwa siku hamsini za Pasaka, Mitume wa Yesu walianza kujiandaa waondoke Yerusalemu ili kwenda kueneza ujumbe wa Kristo.

Mapokeo ni kwamba sehemu ya maandalizi hayo ilikuwa kufunga na kusali ili kupata msaada wa Mungu katika umisionari.

Msingi wa mfungo huo katika Injili ni kwamba, Mafarisayo walipowalaumu mitume hao kwa kutofunga pamoja nao, Yesu alijibu, "Wanawezaje marafiki wa Bwanaarusi kuomboleza, wakati Yeye yuko nao? Lakini siku zitakuja ambazo wataondolewa Bwanaarusi, ndipo watakapofunga."[2]

Maana ya maneno hayo ilihusu Mateso na Kifo chake, lakini kwa namna nyingine iliweza kutafsiri kuhusiana na Kupaa Bwana mbinguni, alipowaagiza kwenda ulimwenguni kuhubiri, jambo linalodai sala na mfungo.

Mapokeo hayo yanashuhudiwa na Papa Leo I (461 KK) katika hotuba zake[3], lakini baadaye yalisahauliwa na Ukristo wa Magharibi kwa kiasi kikubwa.

Inafikiriwa kwamba mfungo huo ulianza kama shukrani kwa Mungu kwa ushuhuda wa Mitume uliofikia hatua ya kufia dini.

  1. Bulgakov, Sergei, Handbook for Church Servers, Movable Feasts and Other Church Seasons Archived 23 Januari 2020 at the Wayback Machine., (Kharkov, Ukraine, 1900),
  2. Math 9:15: taz. Mk 2:19-20, Lk 5:34-35
  3. Pope Leo I of Rome, Sermon 78: On the Whitsuntide Fast

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mfungo wa Mitume kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.