Epifania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mwaka wa Kanisa kadiri ya kalenda ya liturujia ya Roma kama kielelezo cha kawaida kwa Wakristo wa magharibi.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki

Neno epifania linatokana na Kigiriki ἐπιφάνεια, epifaneia, yaani udhihirishaji, tokeo, ujio, uwepo wa Mungu.

Kwa kifupi zaidi 'Eπιφάνια (Yohane Krisostomo) linamaanisha "Kuzaliwa kwa Yesu Kristo", kwa kuwa ndivyo Bwana alivyotutokea.

Kwa kawaida Epifania inaeleweka kama sikukuu muhimu mojawapo ya Ukristo ambayo inahusiana na Noeli na inaadhimishwa kimapokeo tarehe 6 Januari.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Neno ἐπιφάνεια lilitumiwa na Wagiriki kumaanisha tendo ambalo mungu mmojawapo aliweza kujidhirisha kwa binadamu (kwa miujiza, njozi, ishara, n.k.).

Katika karne III Wakristo walianza kulitumia kuhusu matendo ambayo Yesu alijidhirisha (kama vile miujiza yake, ishara n.k.).

Kwa namna ya pekee, kati ya matendo hayo yalisisitizwa: ujio wa mamajusi, Ubatizo wa Yesu na muujiza wake wa kwanza kwenye arusi ya Kana.

Wakatoliki wanasisitiza zaidi ujio wa mamajusi, kumbe Waorthodoksi wanasisitiza ubatizo wa Yesu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]