Kipindi cha Noeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwaka wa Kanisa kadiri ya kalenda ya liturujia ya Roma kama kielelezo cha kawaida kwa Wakristo wa magharibi.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki

Kipindi cha Noeli au Krismasi ni majira ya mwaka wa Kanisa ambapo kadiri ya kalenda ya liturujia ya madhehebu mengi ya Ukristo linaendelea kuadhimishwa fumbo la Krismasi, yaani mwana wa Mungu kuzaliwa kama mtu duniani.

Kipindi cha Noeli katika liturujia ya Roma[1][hariri | hariri chanzo]

Katika kipindi kifupi cha Noeli tunaadhimisha miaka yote ya maisha yaliyofichika ya Yesu Kristo hadi ubatizo wake, alipokabili utume wake mgumu.

Kwanza kwenye sherehe yenyewe tunaadhimisha kuzaliwa kwake katika unyonge wa ubinadamu wetu na katika ufukara wa pango.

Sherehe hiyo inachukua siku nane (Oktava) zinazohesabiwa kuwa moja.

Katikati inaadhimishwa Familia takatifu kama mazingira ya kufaa kwa kumpokea huyo Mwana na kama kielelezo kwa familia zote za binadamu.

Siku ya nane ni pia mwanzo wa mwaka mpya ambao tunaomba uwe na amani. Ndiyo siku ya Yesu kutahiriwa na kupewa jina hilo linaloeleza maana ya yeye kujifanya mtu (ישוח = Mungu anaokoa). Lakini hasa tunamshangilia Bikira Maria mzazi wa Mungu, sifa yake bora iliyompatia fadhili nyingine zote.

Inafuata sherehe ya Epifania (Tokeo la Bwana) ambapo mwanga wa Kristo uliwafikia watu wa mataifa (mamajusi).

Siku ya mwisho unaadhimishwa Ubatizo wa Bwana.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. kama inavyofuatwa Kenya na Tanzania; taz. Misale ya Waamini, toleo la mwaka 2021, uk. 61-62

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kipindi cha Noeli kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.