Mwaka mpya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mianga ya Mwaka Mpya mjini Sydney (Australia)
Mwaka 2022 katika kalenda nyingine
Kalenda ya Gregori 2022
MMXXII
Kalenda ya Kiyahudi 5782 – 5783
Ab urbe condita (Roma ya Kale) 2775
Kalenda ya Ethiopia 2014 – 2015
Kalenda ya Kiarmenia 1471
ԹՎ ՌՆՀԱ
Kalenda ya Kiislamu 1444 – 1445
Kalenda ya Kiajemi 1400 – 1401
Kalenda za Kihindu
- Vikram Samvat 2077 – 2078
- Shaka Samvat 1944 – 1945
- Kali Yuga 5123 – 5124
Kalenda ya Kichina 4718 – 4719
辛丑 – 壬寅

Mwaka mpya ni siku ya kwanza ya mwaka na mara nyingi ni sherehe na nafasi ya watu kutakiana heri na baraka za mwaka mpya.

Katika tamaduni mbalimbali nafasi hii ni sikukuu moja au zaidi pasipo na kazi za kawaida.

Tarehe mbalimbali kufuatana na kalenda tofauti[hariri | hariri chanzo]

Tarehe ya mwaka mpya inategemea kalenda yake. Kuna kalenda tofautitofauti zinazotumiwa dunani na kila moja ina mwaka wake wa pekee pamoja na siku tofauti ya kuanza, mfano kalenda yya kiraia, kalenda ya Kiislamu, mwaka wa Kanisa.

1 Januari[hariri | hariri chanzo]

Kalenda inayotumiwa zaidi kimataifa ni Kalenda ya Gregori na hapa mwaka mpya ni 1 Januari.

Sikusare machipuo[hariri | hariri chanzo]

Uajemi, Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Azerbaijan, Turkmenistan na Kashmir husheherekea mwaka mpya kufuatana na kalenda ya Kiajemi kwenye sikukuu ya Nouruz ambayo ni sawa na sikusare ya machipuo inayotokea kati ya tarehe 20 - 21 Machi kwenye kalenda ya Gregori lakini kwao mwezi na mwaka mpya unaanza

Mwezi mwandamo baada ya solistasi[hariri | hariri chanzo]

Wachina na Wavietnam husheherekea mwaka mpya wakati wa mwezi mwandamo wa pili baada ya solistasi ya Desemba na tarehe hii inatokea kati ya 21 Januari na 21 Februari.

Mwaka wa Kiyahudi[hariri | hariri chanzo]

Nchi ya Israeli na Wayahudi husheherekea mwaka mpya kufuatana na Kalenda ya Kiyahudi kwa jina la Rosh Hashana ambayo ni siku inayotokea kati ya Septemba na nusu ya kwanza ya Oktoba.

Mwaka wa Kiislamu[hariri | hariri chanzo]

Waislamu na nchi ya Saudia huwa na mwaka mpya kufuatana na kalenda ya Kiislamu. Kalenda hii inafuata Mwezi si Jua na kwa hiyo sikuu zake huzunguka katika mwaka wa jua. Hakuna desturi ya kusheherekea mwaka mpya wa Kiislamu.

Diwali[hariri | hariri chanzo]

Sikukuu ya Diwali inasheherekewa na jumuiya kadhaa za Wahindu pia kama mwaka mpya.

Miaka ya kibiashara na kishule[hariri | hariri chanzo]

Nje ya mahesabu haya kuna kalenda nyingine zisizoanzisha mwaka kwa sherehe. Mifano ni:

  • mwaka wa shule
  • mwaka wa biashara ambako hesabu mpya inaanzishwa
  • mwaka wa kanisa ambayo katika sehemu kubwa ya Ukristo unaanza kwenye jumapili ya Adventi (majilio) ya kwanza.
Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwaka mpya kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.