Nenda kwa yaliyomo

Kirgizia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kyrgyzstan)
Jamhuri ya Kirgizia
Кыргыз Республикасы (Kikirigizi)
Кыргызская Республика (Kirusi)
Wimbo wa taifa: Кыргыз Республикасынын Мамлекеттик гимни
Wimbo wa Taifa wa Jamhuri ya Kirgizia
Mahali pa Kirgizia
Mji mkuu
na mkubwa
Bishkek
Lugha rasmiKikirigizi (ya taifa), Kirusi (rasmi)
Lugha ya taifaKikirigizi, Kirusi
  Rais
Sadyr Japarov
  Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri
Adylbek Kasymaliev
Historia
  Uhuru kutoka USSR
31 Agosti 1991
  Uhuru watambuliwa
26 Desemba 1991
  Katiba ya sasa
11 Aprili 2021
Eneo
  Jumlakm2 200,105 (ya 85)
  Maji (asilimia)3.6%
Idadi ya watu
  Kadirio la 20247,200,000
  Msongamano37/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2024
  Jumla $55.2 bilioni
  Kwa kila mtu $7,744
PLT (Kawaida)Kadirio la 2024
  Jumla $17.5 bilioni (ya 126)
  Kwa kila mtu $2,500
HDI (2022) 0.701
- juu
Gini (2022)26.4
SarafuSom ya Kirgizia (KGS)
Majira ya saaUTCUTC+6 (KGT)
Msimbo wa simu+996
Jina la kikoa.kg

Kirgizia, (pia Kirgizstan, Kirigizistani au Kigistani; kwa Kikirgizi: Кыргызстан (Kyrghyzstan); kwa Kirusi: Киргизия (Kirgizia)) rasmi kama Jamhuri ya Wakirgizi, ni nchi isiyo na pwani iliyoko katika Asia ya Kati. Inapakana na Kazakhstan kaskazini, Uzbekistan magharibi, Tajikistan kusini, na China mashariki. Ina idadi ya watu takriban milioni 6.7, ikiwa ya 107 duniani. Mji mkuu na jiji kubwa zaidi ni Bishkek. Kirgizia imegawanyika katika mikoa 7 na jiji kuu moja. Inajulikana kwa milima ya Tian Shan, urithi wake wa maisha ya kuhamahama ya jadi, utamaduni wa Wakyrygyz unaojumuisha muziki wa jadi, mashairi ya simulizi kama Manas, na historia yake kama sehemu ya Njia ya Hariri (Silk Road).

Neno "Kirgizia" linamaanisha "nchi ya makabila 40" kwa lugha ya Kikirgizi. Ukweli ni kwamba kwa sasa yako 80 na zaidi.

Ramani ya Kirgizia

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Hadi mwaka 1991 Kirgizia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet, ikijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikirgizi".

Ilipata uhuru wake katika mwendo wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti.

Kabla ya uhuru yalitokea mabadiliko katika uongozi wa chama cha kikomunisti. Viongozi wapya waliotafuta njia bila udikteta mkali walishika uongozi na rais Askar Akayev alirudishwa madarakani katika uchaguzi wa kwanza na wa pili.

Lakini uchaguzi wa mwaka 2005 ulionekana haukuwa huru, hivyo hasira ya wananchi ikalipuka katika mapinduzi. Uchaguzi mpya ukamteua mpinzani wa awali Kurmanbek Bakiyev.

Ramani ya mikoa ya Kirgizia

Hii ni orodha ya mikoa ya Kirgizia pamoja na makao makuu yake:

  1. Bishkek (mji)
  2. Mkoa wa Batken (Batken)
  3. Mkoa wa Chuy (Bishkek)
  4. Mkoa wa Jalal-Abad (Jalal-Abad)
  5. Mkoa wa Naryn (Naryn)
  6. Mkoa wa Osh (Osh)
  7. Mkoa wa Osh Mjini (mji)
  8. Mkoa wa Talas (Talas)
  9. Mkoa wa Issyk Kul (Karakol)

Demografia

[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya wakazi ilihesabiwa 2005 kuwa watu 5,264,000. Takriban 72.6 % kati yao ni Wakirgizi wenyewe, ambao ni jamii ya Waturuki halafu kuna Wauzbeki (14.4 %) hasa kusini na Warusi (6.4 %) hasa kaskazini, mbali na makundi madogo zaidi.

Lugha ya kawaida ni Kikirgizi, ambacho ni lugha rasmi pamoja na Kirusi. Angalia pia orodha ya lugha za Kirgizia.

Takriban 64% ni Waislamu, lakini kuna uhuru wa dini. Wakristo wako hasa katika ya wakazi wenye asili ya Ulaya, wakiwemo kwanza Waorthodoksi, halafu Waprotestanti na Wakatoliki wachache.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Issyk Kul Lake

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
General information
Ramani
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kirgizia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.