Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Kirgizia

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jina la nchi

[hariri chanzo]

Nimesita wakati wa kutunga kuhusu jina la nchi. Mapendekezo ya BAKITA na TUKI (Kirigizistani na Kigistani) hayaridhiki: ni majaribio ya kutunga jina la nchi (isiyowahi kujadiliwa kwa Kiswahili) kwa njia ya kuandika kwa tahajia ya Kiswahili matamshi ya Kiingereza ya neno. Ilhali Waafrika (kama watu wengine wasio wasemaji asilia ya Kiingereza) watakuwa na matamshi tofauti kati yao ya neno lilelile la Kiingereza kufuatana na lugha ya mama au kawaida ya eneo wanakotoka au kama wamejifunza matamshi ya Marekani au Uingereza basi tunaona maumbo tofauti kati ya wataalamu wa TUKI, BAKITA na Redio Tanzania (linganisha orodha la ILSD chini ya "dictionaries - Swahili Specialized Vocabularies - # geography - English - Swahili linaloonyesha mara kwa mara majina tofauti kwa nchi ileile).

Kama hakuna jina ambalo limekuwa kawaida katika matumizi ya Kiswahili nimefuata kwa kawaida jina la nchi yenyewe au umbo lililo karibu. Isipokuwa "kyrgyztan" inaleta matata kwa sababu hakuna neno la Kiswahili linalotumia "y" mbili; "y" yaonyesha hapa sauti ya "i" ya chini (Kituruki "ı" au Kirusi "ы"). Kwa hiyo nimefuata umbo la Kirusi "Kirgizia" kwa sababu Kirusi ni moja kati ya lugha za Kitaifa za nchi yenyewe. Ila tu ningeona sawa vilevile kama tungetumia "Kirgiztan" ambayo ni umbo linalotumia "i" badala ya "y". Jaribio ! --Kipala 12:34, 4 Machi 2007 (UTC)[jibu]