Nenda kwa yaliyomo

Umoja wa Kisovyeti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Umoja wa Kisovyet)
Umoja wa Kisovyeti
Soyuz Sovyetskikh Sotsialisticheskikh Respublik
Bendera Nembo
Kauli Mbiu
Пролетарии всех стран, соединяйтесь! "wafanyakazi wa nchi tuungane"
Wimbo wa taifa
Государственный гимн Союза Советских Социалистических Республик "State Anthem of the Soviet Union"

ukubwa_wa_picha

Eneo la Umoja wa Kisovyeti

Jiji kubwa
(na mji mkuu)
Moscow
Lugha Rasmi Kirusi
Utaifa Msovieti , Msovyeti
Ukubwa wa eneo
Jumla 22,402,200 km²
Asilimia ya maji 12.3 %
Pato la taifa PPP (1990)
Jumla $2.7 Trilioni (ya 2)
Capita 9,000
Pato la taifa (1990)
Jumla $2.7 trilioni (ya 2)
Capita $9,000

Umoja wa Kisovyeti pia (Kisovieti) (kwa Kirusi: Советский Союз, sovyetskiy soyuz, rasmi kama Umoja wa Jamhuri za Kisovyeti za Kijamii) ilikuwa nchi kubwa duniani kati ya 1922 hadi 1991. Mara nyingi illitwa pia Urusi lakini ilijumlisha Urusi pamoja na maeneo mengine yaliyotwaliwa na Urusi katika mwendo wa historia kabla ya kutokea kwa Umoja wa Kisovyeti yaliyoendelea kuwa nchi huru baadaye.

Ilianzishwa katika Mapinduzi ya Urusi ya 1917 ikachukua nafasi ya Milki ya Urusi ya awali. Umoja wa Kisovyeti ulitawaliwa na chama cha kikomunisti. Wakomunisti waliamua kutawala Dola la Urusi la awali kwa muundo wa shirikisho wakaunda jamhuri mbalimbali kufuatana na mataifa ndani ya eneo hili kubwa.

Kikatiba jamhuri hizi zote zilikuwa nchi huria lakini hali halisi zilitawaliwa zote kutoka makao makuu ya chama cha kikomunisti huko Moscow. Katiba ilipata umuhimu tangu 1989 wakati wa mwisho wa utawala wa Wakomunisti ambako jamhuri zote zilitafuta uhuru wao zikaachana na Umoja.

Mwaka 1991 jamhuri wanachama za mwisho Urusi, Belarus na Ukraini ziliamua kumaliza Umoja wa Kisovyeti.

Viongozi

[hariri | hariri chanzo]

Makatibu Wakuu wa Chama cha Kikomunisti

[hariri | hariri chanzo]

Jamhuri za Umoja wa Kisovyeti

[hariri | hariri chanzo]

Jamhuri za Kisovyeti (zote zimekuwa nchi huria)

[hariri | hariri chanzo]
Ramani ya jamhuri za Umoja wa Kisovyeti
  1. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiarmenia imekuwa Armenia
  2. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiazeri imekuwa Azerbaijan
  3. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kibelarus imekuwa Belarus
  4. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiestonia imekuwa Estonia
  5. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kigeorgia imekuwa Georgia
  6. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikazakhi imekuwa Kazakhstan
  7. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikirgizi imekuwa Kirgizia
  8. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kilatvia imekuwa Latvia
  9. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kilithuania imekuwa Lithuania
  10. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kimoldova imekuwa Moldova
  11. Shirikisho la Jamhuri ya Kisovyiet ya Kijamii ya Kirusi imekuwa Urusi
  12. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kitajiki imekuwa Tajikistan
  13. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kizturkmeni imekuwa Turkmenistan
  14. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraini imekuwa Ukraini
  15. Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiuzbeki imekuwa Uzbekistan
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Umoja wa Kisovyeti kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.