Nenda kwa yaliyomo

Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikirgizi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikirgizi
Кыргыз Советтик Социалисттик Республикасы
Киргизская Советская Социалистическая Республика

(Kirgiz Sovyettik Sotsialistik Respublikasi
Kirgizkaya Sovyetskaya Sotsialisticheskaya Respublika)
Bendera ya Kirgizia ya Kisovyeti Nembo la Kirgizia ya Kisovyeti
Jamhuri ya Kikirgizi ndani ya Umoja wa Kisoveti
Jamhuri ya Kikirgizi ndani ya Umoja wa Kisoveti
Wito la Umoja wa Kisovyeti:
Бардык өлкөлордүн

пролетарлары, бириккиле! Bardyk ölkölordyn prolietarlary, birikkilie
(Kikirgizi: Wafanyakazi wa nchi zote muungane!)

Lugha rasmi hali halisi Kikirgizi na Kirusi
Mji Mkuu Frunse (leo: Bishkek)
Kuanzishwa kama Jamhuri
- Jamhuri ndani ya Umoja wa Kisoveti
- kufutwa

1 Februari 1926

5 Desemba 1936

31 Agosti 1991
Eneo

- % maji

198,500 km²
(wa 7 katika Umoja wa Kisovyeti)
3.6%
Wakazi 4,257,800 (sensa 1989)
Msongamano 21.4/km²
Pesa Rubel (рубль)
Kanda za Wakati UTC +5

Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kikirgizi ( Kirusi: Киргизская Советская Социалистическая Республика) ilikuwa kati ya jamhuri wanachama 15 za Umoja wa Kisovyeti hadi 1991. Jina lake liliandikwa kwa Kikirili katika lugha ya Kikirgizi: "Кыргыз Советтик Социалисттик Республикасы" (Kirgiz Sovyettik Sotsialistik Respublikasi). Leo hii imekuwa nchi huru ya Kirgizia.

Ilikuwa jamhuri kubwa ya saba yenye eneo la 198,500 km² ndani ya Umoja wa Kisovyeti. Mji mkuu ulikuwa Frunse inayoitwa leo Bishkek. Tangu Agosti 1991 imekuwa nchi huria ya Kirgizia katika Asia ya Kati.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Eneo la Kirgizia halikuwa na dola lenyewe linalojulikana likatawaliwa kihistoria na Wamongolia halafu na China. Katika karne ya 19 Urusi ulienea katika Asia ya Kati na Kirgizia kuwa sehemu ya milki ya Urusi.

Baada ya mapinduzi ya kikomunisti ya 1917/18 eneo hili liliendelea katika Shirikisho la Jamhuri ya Kisovyiet ya Kijamii ya Kirusi imekuwa Urusi likapewa cheo cha Mkoa wa kujitawala wa Kara Kirgiz halafu kuwa jamhuri ya Kisovyeti ya kujitawala ya Kirgizia ndani ya Jamhuri ya Kirusi. Tangu 1936 ilikuwa jamhuri mwanachama kamili ya Umoja wa Kisovyeti.

Nchi ikaondoka katika Umoja wa Kisovyeti ulipoporomoka mwaka 1991 na kuwa nchi ya Kirgizia.