Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kimoldova
Mandhari
Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kimoldova ilikuwa kati ya jamhuri wanachama 15 za Umoja wa Kisovyeti hadi 1991. Jina lake liliandikwa kwa Kisirili "Република Советикэ Сочиалистэ Молдовеняскэ (republika sovyetike sotsialiste moldovenyaske) au kwa maandiko ya Kilatini: Republica Sovietică Socialistă Moldovenească; kwa Kirusi: Молдавская Советская Социалистическая Республика.
Iliundwa 1940 kutokana maeneo mawili:
- a) sehemu ya Jamhuri ya kujitawala ya Kisovyeti ya Kijamii Moldova iliyokuwa sehemu ya Jamhuri ya Kisovyeti ya Ukraine hadi 1940
- b) eneo la Bessarabia liliowahi kuwa chini ya Urusi hadi 1918 lakini likatwaliwa na Romania baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Mkataba wa Hitler na Stalin wa 1940 ikarudi chini ya Umoja wa Kisovyeti.
Wakazi wa sehemu hii ni hasa Waromania lakini kuna mchanganyiko na Warusi na Waukraine pia.
Wakati wa kuachana kwa Umoja wa Kisovyeti jina likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Moldava lililotangaza uhuru wake 27 Agosti 1991 kuwa Moldova.