Waturuki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Waturuki (kwa Kituruki: Türk, wingi: Türkler) ni jumuiya 70 za watu wanaotumia lugha ya Kituruki au mojawapo ya lugha zilizo karibu.

Kwa maana nyingine ni jina la raia wote wa nchi ya Uturuki. Wakazi wa Uturuki ni milioni 78 hivi, lakini si wote Waturuki kiutamaduni: wengine (20-30%) ni Wakurdi, halafu Waarabu, Waarmenia n.k.

Waliohamia nje ya Uturuki pamoja na watoto wao ni takriban milioni 4: wengi wao wako Ujerumani.

Waturuki walio wengi ni Waislamu Wasunni, lakini kuna tofauti kati yao. Wengine (labda 25%) ni Waalevi ambao ni tawi la Washia.