Nenda kwa yaliyomo

Lugha za Kiturki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Usambaji wa lugha za Kiturki katia Asia

Lugha za Kiturki ni kundi la lugha zaidi ya 30 zinazozungumzwa kutoka Ulaya ya Mashariki hadi Asia ya Kati na watu milioni 210. Zinahesabiwa kuwa sehemu za lugha za Kialtai pamoja na Kichina, Kimongolia, Kijapani na Kikorea. Wasemaji wa lugha za Kiturki husikizana kwa kiasi kikubwa. Lugha ya Kiturki inayojulikana zaidi kimataifa pia yenye wasemaji wengi ni Kituruki cha Uturuki.

Asili ya wasemaji wa lugha za Kiturki inadhaniwa kuwa sehemu za Mongolia. Kati ya karne za 6 hadi 10 walisambaa hadi Asia ya Magharibi na baada ya kutwaa Milki ya Bizanti waliingia pia katika Ulaya ya kusini-mashariki.

Lugha za Kiturki zenye wasemaji wengi

[hariri | hariri chanzo]

Lugha tatu kubwa za kundi hili ni

[hariri | hariri chanzo]

Lugha za Kiturki zenye wasemaji zaidi ya milioni moja:

[hariri | hariri chanzo]


Mifano ya maneno ya lugha za Kiturki

[hariri | hariri chanzo]

Mifano ifuatayo inaonyesha jinsi gani lugha za Kiturki zinavyofanana:

Kiswahili Kiturki
cha Kale
Kituruki Kiturkmeni Kitatari Kikazakhstan Kiuzbeki Kiuiguri
Mama ana anne/ana ene ana ana ona ana
pua burun burun burun boryn murın burun burun
mkono qol kol qol kul qol qo'l kol
barabara jol yol ýol jul zhol yo'l yol
mnene semiz semiz semiz simyz semiz semiz semiz
ardhi topraq toprak topraq tufrak topıraq tuproq tupraq
damu qan kan gan kan qan qon qan
majivu kül kül kül köl kül kul kül
maji suv su suw syw suw suv su
nyeupe aq ak ak ak aq oq aq
nyeusi qara kara gara kara qara qora qara
nyekundu qyzyl kızıl qyzyl kyzyl qızıl qizil qizil
anga kök gök gök kük kök ko'k kök


Makala hiyo kuhusu "Lugha za Kiturki" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.