Kiazeri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Maeneo penye wasemaji wa Kiazeri

Kiazeri (pia: Kiazerbaijani, Kituruki cha Azerbaijani, kwa lugha ya wenyewe: Azərbaycanca, Azərbaycan dili, آذربایجان تورکجه‌سی) ni moja ya lugha za Kiturki ambayo ni karibu na Kituruki chenyewe. Wengine hutofautisha lugha mbili za Kiazeri, yaani Kiazeri ya Kaskazini nchini Azerbaijani inayoandikwa kwa alfabeti ya Kilatini, na Kiazeri ya Kusini nchini Uajemi inayoandikwa kwa alfabaeti ya Kiarabu (angalia hapo chini).

Maeneo lugha inapotumiwa

Lugha inatumiwa katika jamhuri ya Azerbaijan na katika sehemu za magharibi-kaskazini za Uajemi, pamoja na sehemu za Georgia, Uturuki na Urusi. Idadi ya wasemaji ni takriban milioni 30.

Historia ya lugha ya Kiazeri

Chanzo cha lugha kiko katika lahaja za kituruki ya magharibi zilitumiwa na wahamiaji waturuki waliofika Asia ya Magharibi tangu karne ya 10. Waturuki Waosmani walioteka Konstantinopoli waliendeleza lugha yao kama kitiruki cha Kiosmani kilichokuwa baadaye msingi wa Kituruki wa leo.

Lugha ya makabila ya Anatolia mashariki na Uajemi magharibi imeendelea kuwa asili ya Kiazeri. Wasemaji wa Kiazeri walitawala Uajemi tangu mwaka 1500 kwa nasaba ya Wasafawi. Hii ni sababu ya kwamba Kiazari kilipokea maneno mengi kutoka lugha ya Kiajemi na Kiarabu.

Tangu mwaka 1800 Urusi uliteka eneo la Kaukazi na hivyo wasemaji wa Kiazeri waliishi sasa kisehemu katika Dola la Urusi na kisehemu katika milki ya Uajemi. Kiazeri ya Kaskazini kilipokea pia maneno mmengi kutoka Kirusi.

Baada ya mapinduzi ya kirusi Azerbaijan ya Kirusi iliendelea kuwa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiazeri ambako Kiazeri lifanywa lugha ya kitaifa na kukuzwa kama lugha ya kisasa. hapa maandishi ilibadilishwa kwa kutumia alfabeti ya Kikirili. Baada ya uhuru wa Azerbaijan tangu mwaka 1991 serikali ilibadilisha maandishi kuwa kwa herufi za kilatini kama vile Uturuki.

Lakini Kiazeri kinaendelea kuandikwa kwa andishi la Kiarabu nchini Uajemi.

Mifano ya maandishi ya Kiazeri kwa alfabeti tofauti

Yafuatayo ni kifungu cha kwanza katika Azimio la ulimwengu juu ya haki za binadamu kwa lugha ya Kiazeri lakini kwa maandishi tofauti "Watu wote wamezaliwa huru, hadhi na haki zao ni sawa. Wote wamejaliwa akili na dhamiri, hivyo yapasa watendeane kindugu."

Alfabeti ya Kikirili kwa Kiazeri (hadi 1991)

Бүтүн йнсанлар ләјагәт вә һүгуларына ҝөрә азад вә бәрабәр доғулурлар. Онлрын шүурлары вә виҹданлары вар вә бир-бирләринә мүнасибәтдә гардашлыг рунһунда давранмалыдырлар.

Alfabeti ya Kilatini /Kituruki kwa Kiazeri (tangu 1992)

Bütün insanlar ləyaqət və hüquqlarına göre azad və bərabər doğulurlar. Onların şüurları və vicdanları var və bir-birlərinə münasibətdə qardaşlıq ruhunda davranmalıdırlar.

Alfabeti ya Kiarabu jinsi ilivyo kawaida katika Iran

‏بوتون انسانلار حيثيت و حقلر باخميندان دنك (برابر) و اركين (آزاد) دوغولارلار. اوس (عقل) و اويات (وجدان) ييهﺳﻴﺪيرلر و بير بيرلرينه قارشى قارداشليق روحو ايله داورانماليدرلار‎.

(kwa herufi za Kilatini): Bütün insanlar heysiyyət və haqlar baxımından dənk (bərabər) və ərkin (azad) doğularlar. Us (əql) və uyat (vicdan) yiyəsidirlər və bir birlərinə qarşı qardaşlıq ruhu ilə davranmalıdırlar.

Matini ileile kwa Kituruki kwa ulinganifu

Bütün insanlar hür, haysiyet, ve haklar bakımından eşit doğarlar. Akıl ve vicdana sahiptirler ve birbirlerine karşı kardeşlik zihniyeti ile hareket etmelidirler.

Viungo vya nje

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiazeri kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.