Nenda kwa yaliyomo

Kiuzbeki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Enezi la Kiuzbeki: buluu-nyeusi = wasemaji zaidi ya 50%; buluu-nyeupe = wasemaji chini ya 50%

Kiuzbeki ni moja ya lugha za Kiturki za mashariki na lugha ya Kiturki yenye wasemaji wengi katika Asia ya Kati.

Kwa lugha yenyewe kuna majina "O‘zbek tili" kwa mwandiko wa Kilatini, "Ўзбек тили" (uzbek tili) kwa mwandiko wa Kisirili; au "ئۇزبېك تىلى" (o'zbek tili) kwa mwandiko wa Kiarabu.

Wasemaji

[hariri | hariri chanzo]

Kiuzbeki ni lugha rasmi nchini Uzbekistan ambako kuna wasemaji milioni 21.

Wasemaji wengine wa lugha hii wako Tajikistan (milioni 1.2), Afghanistan (milioni 1), Kyrgyzstan (550,096), Kazakhstan (332,017) na Turkmenistan (317,333).

Mwandiko

[hariri | hariri chanzo]

Tangu uenezaji wa Uislamu Kiuzbeki iliandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Mapinduzi ya kibolsheviki yalileta mwandiko wa Kilatini kati ya 1929 na 1940 kwa kuiga mfano wa Uturuki. Lakini tangu 1940 siasa ikabadilika tena na lugha ikahamishwa kwa mwandiko wa Kisirili kama Kirusi.

Tangu uhuru wa mwaka 1991 mipango ilijadiliwa kurudi kwa mwandiko wa Kilatini. Azimio lilifanywa 1995 kutumia alfabeti ya Kilatini. Lakini hadi sasa mwandiko wa Kisirili bado unapatikana. Waislamu wengine wameendelea kutumia herufi za Kiarabu.

Shule zinatakiwa kufundisha miandiko yote mitatu ili vijana waweze kuendelea kusoma maandishi ya miaka ya nyuma.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]