Nenda kwa yaliyomo

Alfabeti ya Kiarabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mwandiko wa Kiarabu)
"al-ABJaDiya al-arabiya" ni namna ya Kiarabu ya kusema "ABC ya Kiarabu"
(A-B-J-D ni herufi nne za kwanza za alfabeti ya Kiarabu).
Nchi zinazotumia alfabeti ya Kiarabu:      kama mwandiko rasmi pekee      kama mwandiko mmojawapo.

Alfabeti ya Kiarabu ni maandishi maalumu ya lugha ya Kiarabu. Nje ya Kiarabu lugha mbalimbali zinaandikwa kwa alfabeti za Kiarabu, hasa lugha za nchi zenye Waislamu wengi, ingawa herufi hizo zilibuniwa kabla ya dini hiyo kuenea. Kati ya lugha hizo kuna Kiajemi, Kikurdi, Kimalay na Urdu. Pengine katika lugha hizo alfabeti kadhaa zinaongezwa au kupunguzwa, kulingana na lugha ilivyo.

Kihistoria hata Kiswahili na Kituruki ziliwahi kuandikwa kwa alfabeti ya Kiarabu.

Kuna herufi 28 za Kiarabu zinazoandikwa kutoka kulia kwenda kushoto. Herufi zote isipokuwa sita zinaunganishwa wakati wa kuandika. Kutokana na tabia hiyo kila herufi inaweza kuonekana kwa maumbo tofautitofauti kiasi kutegemeana na mahali pake mwanzoni, katikati au mwishoni mwa neno.

Kwa kawaida maandishi ya Kiarabu ni ya konsonanti tu bila vokali. Vokali zikiandikwa zinaonekana kama mstari au nukta chini au juu ya herufi zinazoanzisha silabi.

Herufi kuu

[hariri | hariri chanzo]
Umbo la herufi Jina Soma kama Alama za matamshi ya kimataifa
peke yake mwanzoni katikati mwishoni
أ, إ, ؤ, ئ
hamza ’ ‚ [ʔ]
alif ā [aː]
bāʾ b [b]
tāʾ t [t]
ṯāʾ th [θ]
ǧīm / j [ʤ]
ḥāʾ [ħ]
ḫāʾ / ẖ / kh [x]
dāl d [d]
ḏāl ḏ / dh [ð]
rāʾ r [r]
zāy z [z]
sīn s [s]
šīn š / sh [ʃ]
ṣād [sˁ]
ﺿ ḍād [dˁ]
ṭāʾ [tˁ]
ẓāʾ [ðˁ]
ʿayn ʿ / ‘ [ʕ]
ġayn ġ / gh [ɣ]
fāʾ f [f]
qāf q / ḳ [q]
kāf k [k]
lām l [l]
mīm m [m]
nūn n [n]
hāʾ h [h]
wāw w [w]
yāʾ y [jn]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]