Namba za Kiroma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Namba za Kiroma nu mfumo wa namba jinsi ulivyokuwa kawaida wakati wa Roma ya Kale na katika mwandiko wa Kilatini. Mfumo huu unaendelea kutumiwa hadi leo kwa namba za pekee hasa katika muundo wa orodha ambako mgawanyo ni wa ngazi mbalimbali. Ni kawaida kwa kutofautisha watu wenye jina lilelile kwa mfano wafalme au mapapa: Papa Benedikto XVI (=wa 16) au Malkia Elizabeth II (=wa pili).

Herufi za alfabeti kama alama za namba[hariri | hariri chanzo]

Jinsi ilivyo katika lugha mbalimbali hata Waroma walitumia herufi za alfabeti ya Kilatini pia kwa matumizi kama alama za namba.

Alama za kimsingi[hariri | hariri chanzo]

Herufi chache zilitumiwa kwa namba za muhimu zaidi:

I - 1

V - 5

X - 10

L - 50

C - 100

D - 500

M - 1000

Kuunganisha alama za namba[hariri | hariri chanzo]

Kujumlisha alama[hariri | hariri chanzo]

Namba kubwa zaidi huonyeshwa kwa kuandika alama inayotakiwa upande wa kulia lakini kamwe alama ileile mara nne si zaidi ya mara tatu:
I = 1; II = 2; V ni 5 lakini VI ni 6; XX ni 20 lakini XXI ni 21.

Walikuwa na utaratibu wa kutoandika zaidi ya alama tatu ya aina ileile mfululizo. Lakini waliweza kupuuza utaratibu huu pia na kuandika VIIII (9) badala ya IX au XXXX (40) bafala ya XL.

Kupunguza alama[hariri | hariri chanzo]

Namba ndogo zaidi huonyeshwa kwa kuandika alama ndogo upande wa kushoto:
V ni 5 lakini IV ni 4; X ni 10 lakini IX ni tisa

Hapa walifuata utaratibu ufuatao: kuweka I moja au X moja au C moja tu kabla ya alama kuwba zaidi; halafu namba hii yatolewa kwenye namba kubwa:

Mfano: IX=9; LIV=54; XC=90; CD=400; CM=900

I pekee huwekwa kabla ya V au X; X pekee kabla ya L au C; C pekee kabla ya D au M.

Mfano: XCIX (99) lakini siyo IC; CMXCIX (999) lakini siyo IM

Namba mfululizo[hariri | hariri chanzo]

Alama Namba Alama Namba Alama Namba Alama Namba
I 1 XI 11 XXX 30 CC 200
II 2 XII 12 XL 40 CCC 300
III 3 XIII 13 L 50 CD 400
IV 4 XIV 14 LX 60 D 500
V 5 XV 15 LXIX 69 DC 600
VI 6 XVI 16 LXX 70 DCLXVI 666
VII 7 XVII 17 LXX 80 DCC 700
VIII 8 XVIII 18 CX 90 DCCC 800
IX 9 XIX 19 XCIX 99 CM 900
X 10 XX 20 C 100 M 1000