Solistasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Saa za UTC na tarehe za
sikusare na solistasi duniani[1]
event Sikusare machipuo (Machi) Solistasi ya Juni
(ya kaskazini)
Sikusare otomnia (Septemba) Solistasi ya Desemba
(ya kusini)
month Machi Juni Septemba Desemba
Mwaka
Siku Saa Siku Saa Siku Saa Siku Saa
Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia

Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano

2010 20 17:32 21 11:28 23 03:09 21 23:38
2011 20 23:21 21 17:16 23 09:04 22 05:30
2012 20 05:14 20 23:09 22 14:49 21 11:12
2013 20 11:02 21 05:04 22 20:44 21 17:11
2014 20 16:57 21 10:51 23 02:29 21 23:03
2015 20 22:45 21 16:38 23 08:21 22 04:48
2016 20 04:30 20 22:34 22 14:21 21 10:44
2017 20 10:28 21 04:24 22 20:02 21 16:28
2018 20 16:15 21 10:07 23 01:54 21 22:23
2019 20 21:58 21 15:54 23 07:50 22 04:19
2020 20 03:50 20 21:44 22 13:31 21 10:02

Solistasi (pia:solistisi, kutoka ing. solstice[2]) ni jina la siku mbili katika mwaka ambako tofauti kati ya urefu wa mchana na usiku ni kubwa zaidi kuliko siku zingine. Hutokea mara mbili kwa mwaka.

Tarehe ya kwanza ni 20 au 21 Juni na ya pili ni tarehe 21 au 22 Desemba.

Watu wanaoishi sehemu za jirani na ikweta huwa hawatambui tofauti kati ya muda wa mchana na usiku, ila kadri wanavyoishi mbali zaidi upande wa kusini au kaskazini wa ikweta, tofauti huwa kubwa zaidi.

Kwa kawaida kuna tofauti kati ya urefu wa mchana na usiku isipokuwa kwenye ikweta. Karibu na ncha za Dunia muda wa usiku na mchana unaweza kuwa mrefu hadi karibu nusu mwaka lakini kwa kawaida kuna majira ya mchana mrefu na usiku mrefu zinazobadilishana polepole. Mwendo huu unatokea kinyume kwenye nusutufe mbili za Dunia yaani wakati mchana unarefuka kwenye nusutufe ya kaskazi usiku unarefuka kwenye nusutufe ya kusi.

Katika kanda za karibu na ikweta tofauti hizi hazionekani kirahisi lakini kwenye nusutufe za Dunia upande wa kusini na kaskazini ya ikweta zimetambuliwa tangu karne nyingi na zimekuwa siku muhimu kwa makadirio ya kalenda mbalimbali.

Wakati wa solistasi ya Juni, Jua linafika mahali pa juu zaidi kwenye anga wakati wa adhuhuri kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazi ya Dunia, baadaye inaanza kushuka yaani kuonekana chini zaidi angani wakati wa adhuhuri hadi sikusare ya Septemba. Kwa hiyo njia yake angani ni ndefu na hivyo muda wa mchana ni mrefu. Siku hiyo hiyo ya solistasi ya Juni, Jua linafika mahali pa chini angani pawezekanavyo wakati wa adhuhuri kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kusini ya Dunia. Hapa njia yake angani ni fupi hivyo muda wa mchana ni mfupi. Kinyume chake muda wa usiku unabadilika kuwa mrefu au mfupi.

Vivyo hivyo wakati wa solistasi ya Desemba Jua linafika mahali pa juu kwenye anga wakati wa adhuhuri kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kusi ya Dunia, baadaye inaanza kushuka yaani kuonekana chini zaidi angani wakati wa adhuhuri hadi sikusare ya Machi. Siku hiyo hiyo, Jua linafika mahali pa chini angani pawezekanavyo wakati wa adhuhuri kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazi ya Dunia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. United States Naval Observatory (21 September 2015). Earth's Seasons: Equinoxes, Solstices, Perihelion, and Aphelion, 2000–2025.
  2. Asili ni neno la Kigiriki ἡλιοστάσιον hēliostásion "kusimama kwa Jua")