Sikusare

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Sikusare (pia: ikwinoksi[1], ing. equinox) ni siku ambako urefu wa mchana na usiku ni sawa kote duniani.

Hii inatokea mara mbili kila mwaka, mara ya kwanza mnamo 21 Machi (sikusare machipuo) na 23 Septemba (sikusare otomnia).

Katika kanda karibu na ikweta hazionekani kirahisi lakini kwenye nusutufe za dunia upande wa kusini na kaskazini ya ikweta zimetambuliwa tangu karne nyingi na zimekuwa siku muhimu kwa makadirio ya kalenda mbalimbali.

Kwa kawaida kuna tofauti kati ya urefu wa mchana na usiku isipokuwa karibu na ikweta. Karibu na ncha za dunia muda wa usiku na mchana unaweza kuwa mrefu hadi karibu nusu mwaka lakini kwa kawaida kuna majira ya mchana mrefu na usiku mrefu zinazobadilishana polepole.

Kuanzia usawa wa mchana na usiku kwenye sikusare muda wa mchana unarefuka au kupunguka polepole kati ya kufikia ama siku ya mchana mrefu au usiku mrefu unaotokea katikati ya sikusare mbili za mwaka halafu mwendo hutokea kinyume hadi kufikia sikusare tena.

Mwendo huu unatokea kinyume kwenye nusutufe mbili za dunia yaani wakati mchana unarefuka kwenye nusutufe ya kaskazini usiku unarefuka kwenye nusutufe ya kusini.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. kutoka Kiingereza-Kilatini "equinox"; KAST inatumia "sikusare", TUKI-ESD "ikwinoksi"

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]