Sikusare kaskazi
Mandhari
(Elekezwa kutoka Sikusare ya machipuo)
Sikusare kaskazi (pia ikwinoksi kaskazi[1], ing. vernal equinox) ni moja ya sikusare mbili za mwaka yaani siku ya usawa wa muda wa mchana katika maeneo mbali ya kanda ya ikweta.
Sikusare kaskazi ni sikusare ambako kipindi cha usiku mrefu umekwisha na kipindi cha nusu mwaka kinaanza ambako mchana ni mrefu kuliko usiku. Kuongezeka wa muda wa mchana kunasababisha kupanda kwa halijoto hivyo katika nchi zenye majira baridi mimea huanza kuotea majani mapya.
Sikusare kaskazi inakadiriwa kuwa 21 Machi.
Katika kalenda ya Kiajemi (Iran, Afghanistan, Tajikistan) ni sikukuu inayoitwa Noruzi (نوروز nowruz, pia Nauruzi) na kuwa mwanzo wa mwaka mpya ya Kiajemi.