Mwezi mwandamo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Awamu za Mwezi - Mwezi mwandamo ni na. 1 (Nuru ya Jua kutoka kushoto)
Awamu za mwezi kuanzia mwezi mwandamo (1) kupitia hilali (2), robo ya kwanza, nusu mwezi, robo ya tatu, mwezi mpevu (5) hadi mwezi mwandamo tena

Mwezi mwandamo ni awamu la Mwezi ambako hauonekani kwa macho. Awamu hili linatokea kila baada ya siku 29 1/2.

Katika awamu hili Mwezi uko kati ya Dunia na Jua. Hivyo ni nusu ya Mwezi isiyoonekana kutoka Duniani inayopokea nuru ya Jua lakini upande ambao tunatazama uko kivulini.

Hali halisi upande unaotazama Dunia hauko gizani kabisa kwa sababu unapokea kiasi cha nuru inayoakisiwa kutoka uso wa Dunia.