Sherehe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sherehe ya divai huko Soweto, Afrika Kusini (2009).

Sherehe (kutoka neno la Kiarabu) ni sikukuu muhimu inayoendana na shangwe.

Sherehe nyingi zina asili katika dini mbalimbali na zimeathiri sana utamaduni husika. Kati ya sherehe za namna hiyo kuna Diwali ya Mabanyani, Hanukkah ya Wayahudi, Krismasi ya Wakristo na Eid al-Adha ya Waislamu.

Sherehe nyingine zinaadhimisha mwendo wa mwaka, hasa majira, mazao ya kilimo, au matukio ya historia ya jamii husika, kwa mfano ushindi muhimu vitani, n.k.

Sherehe nyingi zinaadhimishwa mara moja tu kwa mwaka, linavyodokeza neno la Kilatini "sollemnitas" (kwa Kiingereza "solemnity").

Katika Ukristo[hariri | hariri chanzo]

Picha takatifu ya Ufufuko, sherehe muhimu kuliko yote kwa Wakristo.

Katika madhehebu ya Kanisa la Roma, jina hilo linatumika katika kalenda ya liturujia kutambulisha sikukuu za ngazi ya juu kabisa zinazoadhimisha mafumbo ya imani na ya maisha ya Yesu Kristo au hata ya watakatifu wake, hasa Bikira Maria.

Baadhi ya sherehe hazina tarehe maalumu, bali zinategemea adhimisho la Pasaka, ambalo katika Ukristo wa magharibi linaweza kuangukia siku yoyote kati ya 22 Machi na 25 Aprili, kadiri ya mwandamo wa mwezi wa kwanza wa majira ya kuchipua.

Sherehe nyingine zinaangukia tarehe ileile kila mwaka, hasa Noeli, tarehe 25 Desemba.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]


Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sherehe kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.