Picha takatifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ngazi ya Kupanda kwa Mungu ni picha ya karne ya 12 inayoonyesha wamonaki wakipanda kwa Yesu mbinguni, Monasteri ya Mt. Katerina, Sinai.
Picha ya Kirusi ya Utatu Mtakatifu iliyoiga ile maarufu ya Andrei Rublev.
Picha ya Mt. Nikolasi iliyochongwa jiweni kati ya karne ya 12 na karne ya 15, Radomysl Castle, Ukraine[1]

Picha takatifu (kwa Kigiriki εἰκών, eikōn "picha"; ing. icon) kwa kawaida ni mchoro unaoheshimiwa kidini hasa katika Ukristo wa Mashariki lakini pia katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo wa Magharibi, kama vile Kanisa la Kilatini.

Mara nyingi picha hizo zinamhusu Yesu, Bikira Maria, watakatifu wengine, malaika na msalaba.

"Sanaa ya Kikristo" inataja kwanza kati ya karne ya 2 na karne ya 3 katika maandishi ya Tertuliani (160 hivi - 220) na Klemens wa Aleksandria (150 hivi - 212).

Matumizi ya picha hizo yalipingwa na baadhi ya Wakristo, hasa wa mashariki, baada ya Uislamu kutokea na kuenea katika maeneo yao.

Hatimaye Mtaguso wa pili wa Nisea (787) ulithibitisha uhalali wa picha hizo na wa heshima ambazo zinapewa, kama ulivyotetewa hasa na mtakatifu Mwarabu Yohane wa Damasko.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Bogomolets O. Radomysl Castle-Museum on the Royal Road Via Regia". — Kyiv, 2013 ISBN 978-617-7031-15-3

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Beckwith, John, Early Christian and Byzantine Art, Penguin History of Art (now Yale), 2nd edn. 1979, ISBN 0-14-056033-5

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Waorthodoksi[hariri | hariri chanzo]

Wakatoliki[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

ChristianitySymbol.PNG Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Picha takatifu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.