Hanukkah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kinara cha Hanukka kinachoitwa Menorah.

Hanukkah ni sikukuu ya Kiyahudi ya siku nane inayopendwa katika familia. Ni kumbukumbu ya kuweka wakfu upya hekalu la Yerusalemu kwenye mwaka 165 KK. Inasheherekewa tarehe 25 mwezi wa Kislevu inayotokea kati ya mwisho wa Novemba hadi mwisho wa Desemba.

Historia ya sikukuu[hariri | hariri chanzo]

Wakati ule Wagiriki waliwahi kuvamia Yerusalemu na kuanzisha ibada za miungu yao katika hekalu hilo pekee la Uyahudi. Kitabu cha kwanza cha Wamakabayo 4, 36-59 inasimulia jinsi gani Yuda Mmakabayo alisafisha hekalu baada ya kushinda Wagiriki na kuiweka wakfu upya, akiamua iwe sikukuu ya kurudiarudia kila mwaka. Sikukuu hiyo ilikwisha kwa muda baada ya Waroma kubomoa hekalu la Yerusalemu kwenye mwaka 70 lakini iliendelea nje ya Israeli na kusambaa kutoka kwa Wayahudi wa Babeli.

Desturi[hariri | hariri chanzo]

Ishara ya Hanukkah ni kuwasha mishumaa, hivyo inaitwa pia “Sikukuu ya taa”. Asili ya desturi hiyo ni hadithi kuwa, wakati wa kusafisha hekalu Wayahudi walikuta “menorah” yaani kinara cha hekalu ikiwa bado iliwaka lakini mafuta yake yalikuwa karibu kwisha. Kuzimika kwa kinara kilichokusudiwa kuwaka mfululizo kwao kulikuwa balaa. Walihitaji kuandaa mafuta mapya na maandalizi yake pamoja na sala na ibada kwa kawaida yalihitaji siku saba. Lakini kwa muujiza, kiasi hicho kidogo cha mafuta kinasemekana kuwa kilidumu kwa siku nane, ili mafuta mapya na safi yalizalishwa wakati huohuo. Kuwasha mishumaa ya Hanukkah kunakumbusha hadithi hiyo.

Kinara cha Hanukkah kina matawi tisa, tofauti na menorah ya hekalu yenye matawi saba. Maana kinara chenye mianga saba inaruhusiwa katika hekalu pekee. Mshumaa wa katikati ni “taa ya utumishi” ambapo nyingine zinawashwa.

Meza ya chakula cha Hanukkah katika nyumba ya Kiyahudi.

Kwenye siku ya kwanza ya Hanukkah, baada ya giza kuanza, mishumaa huwashwa kwenye sinagogi na nyumbani. Mshumaa mmoja siku ya kwanza, mishumaa miwili siku ya pili, mpaka mishumaa yote itawaka siku ya nane. Sherehe hiyo inajumuisha baraka na nyimbo fulani. Maadamu mishumaa inawaka (angalau dakika 30), hakuna kazi inayopaswa kufanywa, lakini vinginevyo kazi inaweza kufanywa wakati wa Hanukkah, kwa kuwa si sikukuu iliyoagizwa katika Biblia. Hanukkah mara nyingi huitwa Sikukuu ya Taa na huadhimishwa na familia na marafiki.

Kuna vyakula vya pekee, michezo ya pekee na zawadi kwa watoto katika familia.

Hanukkah inazingatiwa kwa usiku na siku nane, kuanzia siku ya 25 ya Kislev kulingana na kalenda ya Kiebrania, ambayo inaweza kutokea wakati wowote kutoka mwishoni mwa Novemba hadi mwishoni mwa Desemba katika Kalenda ya Gregori. Tamasha hilo huzingatiwa kwa kuwasha mishumaa ya candelabrum yenye matawi tisa, ambayo kwa kawaida huitwa menorah au hanukkiah. Tawi moja kwa kawaida huwekwa juu au chini ya mengine na mshumaa wake hutumiwa kuwasha mishumaa mingine minane. Mshumaa huu wa pekee unaitwa shammash ( Hebrew: שַׁמָּשׁ‎ ‎ , "mhudumu"). Kila usiku, mshumaa mmoja wa ziada huwashwa na shammash hadi mishumaa yote minane iwashwe pamoja katika usiku wa mwisho wa tamasha. [1] Sherehe nyingine za Hanukkah ni pamoja na kuimba nyimbo za Hanukkah, kucheza mchezo wa dreidel na kula vyakula vinavyotokana na mafuta, kama vile latkes na sufganiyot, na vyakula vya maziwa. Tangu miaka ya 1970, vuguvugu la Chabad Hasidic duniani kote limeanzisha miali ya umma ya menorah katika maeneo ya wazi ya umma katika nchi nyingi. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "How to Light the Menorah". chabad.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 June 2017. Iliwekwa mnamo 6 October 2018.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  2. "JTA NEWS". Joi.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 October 2007.  Check date values in: |archivedate= (help)