Nenda kwa yaliyomo

Mafuta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muundo wa kijumla wa triglyceride, kipengele kikuu cha mafuta ya mboga na mafuta ya wanyama
Oili sintetiki ya gari ikimiminwa.

Mafuta ni jina la kiowevu kizito chochote kisichochanganyikana na maji lakini ni mumunyifu katika vimumunyisho vya kikaboni[1].

Mafuta yote huwa na asili katika mata ogania, kama vile ya wanyama na mimea.

Aina za mafuta

[hariri | hariri chanzo]

Mafuta ogania

[hariri | hariri chanzo]

Mafuta ogania ni kiowevu kilichokolea, kisichomumunyika majini kilicho na misombo yenye harufu tete kutoka katika mimea. Mafuta hayo hayana haja ya kuwa na sifa yoyote maalumu ya kikemikali ya pamoja, zaidi ya kuwasilisha harufu tofauti.

Katika historia, mafuta hayo yalitumiwa na Wagiriki, Waviking n.k. katika vita kwani wao waliamini yaliwafanya kuwa na nguvu zaidi vitani.

Mafuta hayo yanatumika katika manukato, vipodozi na bidhaa za kuogea, kwa kutia harufu katika chakula, vinywaji, uvumba, kaya na bidhaa za usafi.

Mafuta ya madini

[hariri | hariri chanzo]

Mafuta ya madini, inayopatikana katika miamba inayopitika kwa urahisi chini ya ardhi, yana asili kutoka vyanzo vya kikaboni, kama plankton waliokufa, na kukusanyika chini ya bahari katika nyakati za zamani kijiolojia. Kupitia michakato mbalimbali ya kijiokemikali vitu hivyo viligeuka kuwa mafuta ya madini, au mafuta ya petroli na vipengele vyake, kama vile mafuta ya taa, petroli, dizeli na vingine kama hivi. Haya yanajumuishwa kama mafuta ya madini kwa sababu hayana asili ya kikaboni kwenye nyakati za kuwepo binadamu, bali yanatolewa kutoka katika sehemu za kijiolojia chini ya ardhi, kuanzia miamba, hadi mitego ya chini ya ardhi, na michanga.

Dutu nyingine za kimafuta pia zinaweza kupatikana katika mazingira; inayojulikana zaidi kati ya hizo ni lami inayotokea chini ya ardhi au, kama kuna chungu za uvujaji, katika mashimo ya lami.

Petroli na mafuta mengine ya madini (kemikali za kipetroli) yamekuwa kama rasilimali muhimu ya ustaarabu katika nyakati za sasa na mara nyingi yanatajwa kwa neno "mafuta" yenyewe.

Mafuta ya kikaboni

[hariri | hariri chanzo]

Mafuta pia hutolewa na mimea, wanyama na viumbe vingine kupitia michakato ya kikaboni, na mafuta hayo ni ya ajabu katika tofauti zake: katika kemia yanaainishwa kama wax (misombo yenye mali kama ya mafuta ambayo ni imara katika joto la kawaida), lehemu na dutu nyingine za mafuta zinazopatikana katika viumbe hai kama vile lipidi.

Lipidi, kuanzia waxes hadi steroidi ni vigumu kuzipa tabia fulani, na zimekutanishwa katika kundi ambalo karibu tu linazingatia ukweli kwamba zote zinarudisha, au zinakataa kufuta, katika maji, na ingawa hivyo zinachanganyika] vyema katika viowevu vingine ambavyo ni lipidi. Pia zina kiwango cha juu cha kaboni na hidrojeni, na kwa vikubwa zinakosa oksijeni ikilinganishwa na misombo na madini mengine ya kikaboni.

Mafuta sintetiki

[hariri | hariri chanzo]

Mafuta sintetiki ni kiowevu kinachojumuisha misombo ya kemikali yanayotengenezwa (synthesized) kisasa kutoka kwa misombo mingine badala ya mafuta ghafi (petroli). Mafuta sintetiki hutumika kama mbadala wa lubricant iliyosafishwa kutoka kwa mafuta ya petroli, kwa sababu kwa ujumla hutoa mwasho na mali za kikemikali kuu kuliko zile zinazopatikana katika mafuta ya madini ya jadi.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]
Chupa ya mafuta ya zeituni yanayotumika kwa chakula.

Mafuta mengi yanayoweza kulika ya mimea na wanyama hutumiwa katika mapishi na maandalizi ya chakula. Hasa vyakula vingi hukaangwa katika mafuta ya moto kuliko maji yanayochemka. Mafuta pia hutumika kubadilisha harufu na kuongeza ulaini wa baadhi ya vyakula.

Faida za kiafya zinadaiwa kwa idadi ya mafuta maalumu kama mafuta ya omega 3 (mafuta ya samaki, mafuta ya flaxseed, n.k.), mafuta ya evening Primrose na mafuta ya zeituni.

Mafuta ya Trans fats mara nyingi yanayozalishwa kwa kuongeza hidrojeni katika mafuta ya mboga, yanajulikana kuwa na madhara kwa afya.

Mafuta hutumika kwenye nywele kuzipa hali ya kung'aa. Husaidia kuzuia ukwaru na kukunjana kwa nywele. Pia husaidia nywele kuwa tulivu na kukua kwa haraka.

Kulowesha ngozi

[hariri | hariri chanzo]

Mafuta hupakwa katika ngozi ili kuilowesha. Wasichana na akina mama hupenda sana kutumia mafuta ili ngozi yao iwe laini na ing'are kila wakati. Unaponyauka ngozi, inafaa upake mafuta. Kwa walio na ngozi ya kupata chunusi wakichomeka na jua kwa muda mrefu, wanaweza kutumia sunburn oils Ilihifadhiwa 20 Septemba 2020 kwenye Wayback Machine. ili kufanya ngozi ilainike.

Karibu mafuta yote huwaka katika namna ya erosoli na kuzaa joto, ambalo linaweza kutumika moja kwa moja, au kama kiongofu katika aina nyingine ya nishati kwa njia mbalimbali. Mafuta ambayo husukumwa kutoka ardhini husafirishwa kwa matangi ya mafuta hadi kwenye kiwanda cha kusafishia mafuta. Huko, inageuzwa kutoka mafuta ghafi iwe dizeli (petrodiesel), ethane (na alkanes zingine zenye mnyororo mfupi), mafuta ya kutolea nishati, petroli, mafuta ya ndege, mafuta ya taana petroli ya gesi kimiminika.

Uzalishaji wa umeme

[hariri | hariri chanzo]

Mafuta na aina yoyote ya bidhaa zake iliyosafishwa zaidi mara nyingi hutumiwa kutengeneza umeme. Hii inafanywa kwa njia ya injini ya mvuke. Injini ya mvuke inageuza nishati ya joto iwe mizunguko, ambayo yanaweza kugeuzwa kuwa umeme, kwa njia ya jenereta.

Usafirishaji wa joto

[hariri | hariri chanzo]

Aina nyingi za mafuta zina viwango vya juu vya mchemko kushinda maji na ni vihami vya umeme, hili linayafanya kuwa ya manufaa katika michakato ya kupoesha viowevu, hasa pale umeme unapotumika.

Lubrication

[hariri | hariri chanzo]

Kwa kukosa polarity, mafuta hayawezi kuambatana kwa urahisi na dutu nyingine. Hii inafanya mafuta kuwa muhimu kama lubricant katika uhandisi kwa madhumuni mbalimbali. Mafuta ya madini yanafaa zaidi kuliko mafuta ya kibiolojia, ambayo huharibika haraka katika aina nyingi za mazingira.

Upakaji rangi

[hariri | hariri chanzo]

Sera za rangi zinaweza kuelea kwa urahisi katika mafuta, na kuifanya ifae kama kiowevu cha kusaidia kwa rangi. Mchakato wa kukauka polepole na umumunyifu wa mafuta husaidia hali ya kikweli. Njia hii imekuwa ikitumiwa tangu karne ya 15.

Kemikali za kipetroli

[hariri | hariri chanzo]

Mafuta ghafi yanaweza kuundwa kuwa mafuta ya petroli; 'kemikali za kipetroli' ni bidhaa za kikemikali zilizotengenezwa kutoka malighafi ya mafuta ya petroli au asili nyingine ya hidrojeni na kikaboni. Yanatumika katika bidhaa kama vile sabuni, mbolea, madawa, rangi, plastiki, nyuzi sintetiki na mpira sintetiki.

Matumizi mengine

[hariri | hariri chanzo]

Asidi ya sulfuric imeitwa mafuta ya vitriol katika nyakati kabla ya kisayansi, kutokana na kunata kwake. Hata sasa, wakati mwingine inaitwa asidi vitriolic, na haiba caustic wanaitwa "vitriolic". Asidi hiyo si kemikali ya kipetroli, na kisasa, si ya mafuta.

Mafuta zimetumika katika historia kama manukato ya kidini. Mafuta mara nyingi huonekana kama chombo cha utakaso wa roho.

Yanatumika katika ibada, kama vile krisma ambayo hutumika katika ubatizo, kipaimara na daraja takatifu, na kijadi yametumiwa kutawaza mfalme na malkia, lakini pia kuhani katika Agano la Kale (Biblia ya Kiebrania).

Mafuta ambayo inahusishwa na mtakatifu mmoja au zaidi inajulikana kama "mafuta ya watakatifu" na inaaminiwa na baadhi kuwa na manufaa, kama vile "mafuta ya mashahidi" [2]

  1. Emulsifier inaruhusu mafuta na maji kuchanganyika
  2. Kamusi-elezo ya Katoliki: Mafuta ya Watakatifu

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mafuta kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.