Uvumba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Gramu 100 za utomvu kavu ya uvumba
Uvumba kutoka Yemen

Uvumba (pia: Ubani) ni utomvu kavu mwenye harufu ya kupendeza ukichomwa. Inapatikana kutoka miti ya aina Boswellia thurifera (pia: Boswellia sacra).

Matumizi ya kidini[hariri | hariri chanzo]

Matumizi yake ni katika ibada za kidini lakini pia nyumbani. Mataifa ya kale ya Mashariki ya Kati yalitumia uvumba mahekaluni kwa mfano Wamisri, Wayahudi na Waroma wa Kale.

Kutoka kawaida ya Uyahudi lakini pia ya Dola la Roma matumizi yake yameingia katika Ukristo na katika liturgia za Kanisa Katoliki na Kanisa Kirthodoksi. Waprotestanti huwa hawaitumii isipokuwa sehemu za Waanglikana na Waluteri wenye mwelekeo wa kukazia urithi wa kiliturgia.

Matumizi ya kiganga[hariri | hariri chanzo]

Kuna pia matumizi kama dawa ya kumeza kwa kusudi la kuimarisha akili na kumbukumbu lakini pia kwa kupambana na ugonjwa wa jongo. Wamisri wa Kal waliitumia kwa kutunza maiti ya marehemu.

Biashara ya uvumba[hariri | hariri chanzo]

Miti ya Boswellia hustawi katika maeneo yabisi kama Yemen, Omani, Somalia, Ethiopia na sehemu za Bara Hindi mbali na nchi zenye rutba nzuri na watu wengi. Hivyo Uvumba ulitafutwa sana na kufanyiwa biashara kama bidhaa yenye thamani.

Katika taarifa ya Biblia uvuma ilikuwa kati ya zawadi zilizopelekwa Bethelehemu na mamajusi wa mashariki.