Kaboni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta


Kaboni (Carbon)
C-TableImage.png
Jina la Elementi Kaboni (Carbon)
Alama C
Namba atomia 6
Mfululizo safu Halojeni
Uzani atomia 12,0107 u
Valensi 2,4
Kiwango cha kuyeyuka 3820 K (3550 °C)
Kiwango cha kuchemka 5100 K (4800 °C)

Kaboni (ing. carbon) ni elementi yenye namba atomia 6 na uzani atomia 12 kwenye mfumo radidia. Alama yake ni C. Inapatikana pekee yake kwa umbo mbalimbali kama vile makaa au almasi lakini mara nyingi katika michanganyiko ya kikemia.

Kati ya tabia za kaboni ni uwezo wake wa kujiunga na elementi nyingi hivyo kuunda molekuli kubwa.

Kaboni ni elementi muhimu zaidi pamoja na oksijeni katika vyumbehai vyote pamoja na mimea. Iko katika idadi kubwa ya kampaundi ogania.

Kiteknolojia kaboni ni muhimu kwa sababu ni kimsingi wa aloi zote za chumapua na hivyo teknolojia ya kisasa. Kwa upande mwingine kaboni iko pia katika aina zote za plastiki.

Chem template.svg Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kaboni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.