Kiowevu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Anguko la tone laonyesha maumbo mengi ya kiowevu

Kiowevu au kioevu (pia: kimiminika, kimiminiko) ni moja kati ya hali maada.

Katika hali kiowevu atomi zina nafasi ya kuachana na kubadilishana mahali. Kwa sababu hii kiowevu hakina umbo maalumu.

Masi ya kilogramu moja ya maji hukubali umbo la kila chombo kinamomwagwa: ama katika sufuria pana au bomba ndefu nyembamba. Kama maji yaleyale yameganda na kuingia katika hali mango kama barafu hauwezi kukubali umbo tofauti.

Kiowevu hukubali badiliko la umbo lakini hakibadiliki mjao na uzani.

Kiowevu ikifikia kiwango cha kuchemka huingia katika hali ya gesi .

Atomi katika hali maada mbalimbali[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]