Mango

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mango (wakati mwingine pia: yabisi[1]) ni moja kati ya hali maada. Maana yake ni imara, tofauti na kiowevu (majimaji) au gesi (kama hewa).

Katika hali mango atomu zinakaa mahali pamoja katika gimba hazichezi wala kutembea ndani yake. Kila atomu ina mahali pake. Gimba mango lina umbo, mjao na uzani maalumu. Umbo mango lina urefu, upana na kimo chake, tofauti na kiowevu kinachobadilisha umbo kufuatana na chombo chake au gesi isiyo na umbo wala mjao maalumu.

Kama mango inabadilika kuwa kiowevu tunasema inayeyuka. Kama inabadilika kuwa gesi au mvuke moja kwa moja tunaliita badiliko hili mvukemango.

Atomi katika hali maada mbalimbali[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Mango" ni matumizi jinsi yalivyopendekezwa zaidi katika kamusi za TUKI; pia vitabu vipya vya shule za sekondari Tanzania zinavyoandaliwa kwa Kiswahili, kama vile "Jifunze Fizikia", iliyotolewa na Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili, 2015. "Yabisi" inataja zaidi hali ya ugumu kutokana na kukauka.
Science.jpg Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mango kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.