Lipidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lipidi (kwa Kiingereza lipid, kutoka Kigiriki λίπος, lípos, „mafuta“) ni kundi la molekuli ogania zinazojenga dutu kama mafuta, nta na sehemu ya vitamini.

Ni muhimu katika kemia ya viumbehai kwa sababu zinahifadhi nishati ndani ya seli za mwili, zinapitisha habari kati ya seli na kujenga utando wa seli.[1] Kwa hiyo ni sehemu muhimu ya chakula.

Zinapatikana kwa kula algae, mbegu wa mimea, nyama, jibini, siagi na samaki.

Wakati mwingine neno "lipidi" hutumiwa sasa na mafuta lakini hali halisi mafuta ni kundi la lipidi tu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Fahy E. et al (2009). "Update of the LIPID MAPS comprehensive classification system for lipids". Journal of Lipid Research 50 (Supplement): S9–S14. PMC 2674711. PMID 19098281. doi:10.1194/jlr.R800095-JLR200. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lipidi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.