Nenda kwa yaliyomo

Jibini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Soko la jibini mjini Gouda (Uholanzi)
Kiwanda cha jibini ya Parmigiano (Italia)
Aina za jibini huko Basel (Uswisi)

Jibini ni chakula kinachotokana na maziwa.

Maziwa ya ng'ombe, kondoo au mbuzi hugandishwa. Hupikwa katika sufuria na dawa asilia kutoka tumbo la ndama ya ng'ombe (kimeng'enya cha renini) humwagwa humo pamoja na chumvi. Maziwa yanaganda mara moja na kumwagwa katika kitambaa ili majimaji yatoke na hatimaye sehemu imara pekee ibaki.

Jibini mbichi inaweza kukandamizwa na kuwa imara zaidi. Baadaye, ilhali ni bado laini, huwekwa katika bakuli na kupokea umbo lake wakati inaendelea kukauka.

Baadaye inakaa na kuiva. Aina mbalimbali za jibini huiva kwa muda tofautitofauti.

Katika nchi za joto ni vigumu zaidi kutengeneza jibini bila mashine na friji, lakini katika nchi nyingi jibini ni sehemu ya utamaduni. Jibini ni chakula bora chenye protini na mafuta sawa na maziwa. Kiuchumi ni muhimu kama njia ya kutunza maziwa kwa miezi mingi.

Nchi kama Uholanzi, Ufaransa, Uswisi na Italia ni maarufu kwa aina nyingi za jibini, kila moja ikiwa na ladha na rangi tofauti.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jibini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.