Ladha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ladha ni jumla ya hisi zinazopatikana kinywani wakati unapoonja kitu.

Kwa mfano, unaweza kusikia utamu, uchungu, ukali wa chakula au kinywaji fulani ukapendezwa au kutopendezwa nao.

Kiungo kinachohusika zaidi ni ulimi.

Uwezo wa kuonja ladha huhesabiwa kati ya milango ya fahamu.

Kwa kawaida mapishi yanalenga kuridhisha ladha iwezekanavyo. Jambo hilo ni muhimu hasa kwa wagonjwa wasio na hamu ya chakula. Hata hivyo, ni hatari kwa walafi kwa kuwa linawafanya wale kuliko mahitaji ya mwili na hivyo kuchangia uharibifu wa afya.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ladha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.