Milango ya fahamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Macho, pua na nywele ndefu za "ndevu" ni milango muhimu kwa huyu paka.

Milango ya fahamu ni ogani za mwili zinazoturuhusu kujua mazingira yetu. Mifano yake ni macho na masikio. Ni njia asili ya kutambua mtazamo au hisia.

Kibiolojia inaelezwa kuwa ogani yenye uwezo wa kupokea habari za nje ya mwili, kama vile nuru, sauti, halijoto, mwendo, harufu au ladha, na kuzibadilisha katika mishtuko ya umeme inayofikishwa kwa njia ya mfumo wa neva hadi ubongo.

Kama milango ya fahamu imeharibika, tunasema mtu ni kipofu, bubu au kiziwi, ana matatizo kuelewa mazingira yake sawa na jinsi wanavyoweza watu wengine.

Milango ya fahamu ni muhimu sana kwa Viumbe hai kutokana na kwamba inasadia kiumbe hai katika shughuli zake za kila siku, hasa katika kufatuta mahitaji muhimu (kwa Kiingereza yanaitwa Basic needs).

Fahamu zetu[hariri | hariri chanzo]

"Fahamu tano za binadamu" kadiri ya mchoraji Mwaustria Hans Makart (1840-1884).

Mara nyingi watu hutaja fahamu tano([1] [2]) ambazo ni:

  1. Kusikia ni fahamu ya sauti kupitia masikio
  2. Kuona ni fahamu ya nuru kupitia macho
  3. Kuonja ni fahamu ya ladha kupitia ulimi
  4. Kunusa ni fahamu ya harufu kupitia pua
  5. Mguso ni fahamu ya nyuso za vitu kupitia ngozi, hasa ya mkono

Hali halisi kuna fahamu zaidi:

  1. Fahamu ya joto - baridi
  2. Fahamu ya maumivu
  3. Fahamu ya uwiano (inayotuwezesha kusimama, kutofautisha juu na chini)
  4. Fahamu ya mwili wetu (inayotuwezesha kugusa pua wakati macho yamefungwa)

Mfumo wa kibiolojia ya fahamu zetu[hariri | hariri chanzo]

Ogani mbalimbali za mwili ziko tayari kupokea vichocheo kutoka mazingira yetu.

Neva katika ogani husika zina uwezo wa kupokea vichocheo vya nje vinavyotafsiriwa katika ubongo kwa fahamu mbalimbali

  1. vichocheo vya kikemia vinavyotuwezesha kuonja na kunusa[3]
  2. vichocheo vya nuru vinavyotuwezesha kuona[4]
  3. vichocheo vya halijoto vinavyotuwezesha kutofautisha joto na baridi[5]
  4. vichocheo vya shinikizo na mwendo[6]
  5. vichocheo vya athari hatari vinavyotafsiriwa na ubongo kwa maumivu au kichefuchefu[7]

Wanyama pia wana ogani zinazowawezesha kutambua:

  1. vichocheo vya kusumaku (kwa mfano ndege wanaohamahama mbali kila mwaka kwa kufuata uga wa sumaku wa dunia)
  2. vichocheo vya umeme
  3. vichocheo vya mnururisho sumakuumeme nje ya nuru ya kawaida, kwa mfano nyuki hutambua mawimbi ya urujuanimno yasiyoonekana na binadamu

Picha za milango ya fahamu[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://en.wikipedia.org/wiki/Five_senses_(disambiguation)
  2. https://en.wiktionary.org/wiki/five_senses
  3. Satir,P. & Christensen,S.T. (2008) Structure and function of mammalian cilia. in Histochemistry and Cell Biologygfgh, Vol 129:6
  4. Foster, R. G.; Provencio, I.; Hudson, D.; Fiske, S.; Grip, W.; Menaker, M. (1991). "Circadian photoreception in the retinally degenerate mouse (rd/rd)". Journal of Comparative Physiology A 169
  5. Krantz, John. Experiencing Sensation and Perception. Archived 17 Novemba 2017 at the Wayback Machine. Pearson Education, Limited, 2009. p. 12.3
  6. Winter, R., Harrar, V., Gozdzik, M., & Harris, L. R. (2008). The relative timing of active and passive touch. [Proceedings Paper]. Brain Research, 1242, 54-58. doi:10.1016/j.brainres.2008.06.090
  7. International Association for the Study of Pain: Pain Definitions [Retrieved 10 Sep 2011]. "Pain is an unpleasant sensory and emotional experience associated with actual or potential tissue damage, or described in terms of such damage" Derived from Bonica JJ. The need of a taxonomy. Pain. 1979;6(3):247–8
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Milango ya fahamu kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.