Anatomia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mondino dei Liuzzi, Anathomia, 1541

Anatomia (pia anatomi[1], en:anatomy, kutoka Kigiriki ἀνατέμνειν anatemnein - kupasua, kufungua) ni elimu ya miili ya viumbehai kama binadamu, wanyama na mimea. Inachungulia muundo na umbile la mwili na sehemu au viungo vyake.

Wataalamu wa anatomia hufungua mwili na kuikata kwa sehemu zake kwa kusudi la kuongeza elimu ya muundo wake.

Elimu hii inasaidia kuelewa magonjwa, pamoja na sababu na matokeo yake. Ni pia msingi wa mafundisho ya tiba na elimu ya matibabu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Anatomi ni pendekezo la KyT kutokana na matamshi ya Kiingereza

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Anatomia kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.