Zoolojia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Aina nyingi za wanyama

Zoolojia (tamka zo-o-lo-jia, kutoka gir. ζῷον zóon "mnyama, kiumbe hai" na λόγος logos, "neno, fundisho“) ni tawi la biolojia linalochunguza wanyama, hasa wanyama wenye seli nyingi (metazoa).

Zoolojia linatumia mbinu mbalimbali za kisayansi likichungulia maumbile na miili ya wanyama, michakato ndani ya miili, historia ya mageuko ya spishi za wanyama, jenetiki yao, usambazaji wao katika maeneo ya dunia, uhusiano wao na mazingira (ekolojia) na jinsi gani wanyama wanahusiana kati yao. Zoolojia imeunda mfumo wa kupanga wanyaa wote kwa vikundi (uainishaji wa kisayansi) na kuendelea utaratibu huu.

Wanazoolojia kwa kawaida hufuata masomo ya biolojia na kwenye ngazi za juu zinaweka mkazo upande wa elimu ya wanyama. Wanafanya kazi kwenye vyuo vikuu, katika maabara ya makampuni ya madawa, katika bustani za zoo au katika makumbusho.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Kigezo:Wiktionarycat