Vitamini
Vitamini ni kirutubishi kinachohitajika na mwili kwa kujenga afya yake. Kwa lugha nyingine kampaundi ogania zilizo lazima kwa shughuli za mwili lakini haziwezi kutengenezwa na mwili mwenyewe hivyo ni lazima kuzipata kupitia chakula. Vitamini inaitwa mara nyingi kwa herufi kama vitamini A, vitamini B, vitamini C na kadhalika. Vitamini C hupatikana hasa kwenye matunda kama limau au chungwa.
Vitamini hutofautiana kati ya viumbe maana kama kemikali huitwa "vitamini" inategemea kama kiumbe fulani anaweza kutengeza kemikali hii ndani ya mwili wake au la. Kwa mfano vitamini C ni asidi askobini na wanyama wengi wanaitengeneza ndani ya miili yao; lakini sehemu ya mamalia hasa nyani wakubwa (primates) pamoja na binmadamu hawawezi kuitengeneza hivyo wanahitaji chakula chenye asidi hii.
Viumbe wanaweza kuishi bila matata wakikosa vitamini kwa muda mfupi lakini uhaba wa muda mrefu unaleta magonjwa.
Leo hii vitamini nyingi kwa mahitaji ya binadamu hutengenezwa viwandani na kupatikana kama vidonge.
Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]
-->