Nenda kwa yaliyomo

Vitamini C

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
ascorbic acid
Viazi katika ganda huwa na 20 mg/100 g za vitamini C

Vitamini C ni vitamini inayopatikana hasa katika matunda na majani mabichi. Kikemia ni aina ya asidi askobini na binadamu ni kati ya spishi chache ambazo haziwezi kutengeneza asidi hii mwilini. Kwa hiyi watu hutegemea chakula chenye kiwango cha vitamini hii.

Vitamini C ina kazi muhimu katika mchakato wa kupona vidonda mwilini. Uhaba wake kwa muda mrefu unasababisha ugonjwa wa kiseyeseye (au hijabu). Kiseyeseye husababisha ufizi wa meno kuwa na vidonda na pia vidonda vingine mwilini kutopoa. Ugonjwa huu ulijulikana hasa wakati wa safari ndefu za baharini. Zamani haikujulikana chanzo chake kilikuwa nini; meli na jahazi zilibeba tu unga wa mkate au mchele kama chakula kilichoongezwa kwa nyama kavu au samaki kutoka baharini lakini matunda hayakuwa kawaida. Mabaharia wengi waligonjeka na kufa. Katika karne ya 19 mabaharia walitambua ya kwamba akiba ndogo ya malimau inaweza kuokoa watu kama wanakunjwa kijiko cha maji ya limau kila baada ya siku kadhaa.

Mwaka 1928 vitamini C iligundiuliwa pia kikemia na tangu 1928 ilithibitishwa kuwa inasmimamisha kiseyeseye.

Mahitaji ya mwili hukadiriwa kuwa miligramu 60-100 kwa siku; kiwango hiki kinapatikana kwa njia ya chakula cha kawaida.

Matunda kama limau, chungwa na balungi ni vyanzo bora vya vitamini C. Kwa jumla karibu matunda yote yenye ladha ya kichungu ni chanzo chake.

Kuna pia aina za nyama na samaki zinazopeleka vitamini C mwilini. Hapo ndipo sababu ya kwamba Waeskimo hawakuwa na kiseyeseye ingawa zamani waliishi bila matunda kwa miezi mingi lakini walikula samaki bichi.

Kupika chakula kwa muda mrefu kunaharibu asidi ya vitamini C.


Jedwali inayoonyesha kiwango cha Vitamini C katika matunda na mboga
Matunda mg vitamini C kwa kila gramu 100 za tunda Matunda mg vitamini C kwa kila gramu 100 za tunda Matunda mg vitamini C kwa kila gramu 100 za tunda
CamuCamu2800Limau 40Mizabibu10
Rose hip2000Melon, cantaloupe 40Apricot10
Acerola1600Cauliflower 40Plum10
Jujube500Grapefruit 30Watermelon10
Baobab400Raspberry 30Ndizi9
Blackcurrant200 Tangerine/ Mandarin oranges 30Karoti9
Indian gooseberry445Passion fruit 30Avocado8
Guava100
Kiwifruit90Spinach 30Crabapple8
Broccoli90Cabbage Raw green 30Peach7
Loganberry80Lime 20Tofah6
Redcurrant80Mango 20Blackberry6
Brussels sprouts80Melon, honeydew 20Beetroot5
Lychee70Raspberry 20Pear4
Persimmon60nyanya 10Lettuce4
Papaya60Blueberry 10Cucumber3
Strawberry50mananasi 10Fig2
Orange50Pawpaw10Bilberry 1
+ Jedwali inayoonyesha kiwango cha Vitamini C katika nyama na samaki
Aina ya nyama mg vitamini C kwa gramu 1000 za chakula Aina ya nyama mg vitamini C kwa gramu 1000 za chakula Aina ya nyama mg vitamini C kwa gramu 1000 za chakula
Ndama maini (bichi)36Kuku maini (fried ) 13Mbuzi maziwa (bichi)2
ng’ombe maini (bichi)31Kondoo maini (ya kuchoma) 12NYama ya ng’ombe nyekundu (ya kuchoma)0
Oysters (bichi)30Lamb heart (ya kuchoma) 11Mayai ya kuku (bichi )0
Cod Roe (ya kuchoma)26Kondoo ulimi (stewed) 6Nyguruwe Bacon (ya kuchoma)0
Nguruwe maini (bichi)23 Maziwa ya binadamu (bichi) 4Nyama ya ndama (ya kuchoma)0
Lamb brain (ya kupikwa)17 Cows maziwa (bichi)2Chicken leg (ya kuchoma) 0