Kupaa Bwana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kupaa Kristo kadiri ya Garofalo, 1520.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki

Sherehe ya Kupaa Bwana ni ukumbusho wa fumbo la Yesu Kristo kupaa katika utukufu wa mbinguni akiwa na mwili wake ambao ulisulubiwa hata akafa akazikwa kabla hajafufuka siku ya tatu kadiri ya imani ya Ukristo.

Ni adhimisho linalounganisha madhehebu mengi sana katika kumshangilia Yesu kufanywa Bwana.

Kwa kawaida sikukuu hiyo inafanyika siku 40 baada ya Jumapili ya Pasaka kufuatana na hesabu ya Matendo ya Mitume 1:3, ingawa pengine inasogezwa kutoka Alhamisi hadi Jumapili ijayo ili kuwawezesha waamini wote kushiriki pale ambapo siku yenyewe ni ya kazi, si sikukuu ya taifa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Adhimisho hilo ni la zamani sana. Ingawa hakuna uthibitisho wa kimaandishi kabla ya mwanzo wa karne ya 5, Agostino wa Hippo alisema linatokana na Mababu wa Kanisa wa kwanza, na kwamba linafanyika katika Kanisa lote tangu muda mrefu.

Kweli linatajwa mara nyingi katika maandishi ya Yohane Krisostomo, Gregori wa Nisa, katika Katiba za Mitume na mengineyo ya Makanisa ya mashariki na Kanisa la magharibi.

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: