Nenda kwa yaliyomo

Ravenna

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu ya mji


Ravenna
Nchi Italia
Mkoa Emilia-Romagna
Wilaya Ravenna
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 134,631
Tovuti:  www.comune.ravenna.it

Ravenna ni mji wa Italia katika mkoa wa Emilia-Romagna. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2009, kuna wakazi wapatao 135.000 wanaoishi katika mji huu. Mji upo m 4 juu ya usawa wa bahari.

Ravenna ni mashuhuri duniani kwa majengo yake ya kale ambayo ni mifano bora wa sanaa ya Kikristo ya karne za 5 na 6 BK. Kuna majengo 8 ya Ravenna yaliyoingizwa katika orodha ya UNESCO ya urithi wa dunia.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kati ya 402 hadi 476 Ravenna ilikuwa makao makuu ya kaisari na hivyo mji mkuu wa Dola la Roma la Magharibi. Baada ya mwisho wa utawala wa Kiroma katika magharibi iliendelea kuwa mji mkuu wa wafalme wa Kigermanik kama Odoaker na Theodoriki. Wagermanik walikuwa Wakristo wa dhehebu la Waariano lakini wakazi wenyeji wa mji walifuata Ukristo wa Kiorthodoksi. Baada ya Italia kurudishwa chini ya Dola la Roma la Mashariki mji ulikuwa makao makuu ya gavana mkuu wa Bizanti katika Italia hadi mwaka 751 ambako kabila la kigermanik la Walangobardi lilitawala tayari sehemu kubwa za Italia ya Kaskazini lilivamia pia Ravenna. Wakati ule Walangobardi walikuwa Wakatoliki na katika miaka iliyofuata Wakristo wa Ravenna walikuwa chini ya usimamizi wa Papa wa Roma.

Urithi wa dunia

[hariri | hariri chanzo]

Majengo yaliyo maarufu leo yalijengwa katika karne hizi za Ravenna kuwa mji mkuu wa Italia. Makanisa yote yamepambwa kwa mozaiki nzuri ukutani.

  • Kanisa la San Vitale (karne ya 6)
  • Kaburi kwa malkia Galla Placidia (karne ya 5); ilijengwa kwa umbo la kanisa dogo; malkia haikuzikwa hapa bali mjini Roma lakini inaaminiwa ya kwamba malkia aliandaa jengo hili kuwa kaburi lake.
  • Kanisa la Sant’Apollinare Nuovo (karne ya 6); hii ilikuwa kanisa kwa ajili ya mfalme Theodoriki ambako ibada zilisheherekewa kufuatana na liturgia ya Waariano.
  • Kaburi la Theodoriki; lina paa yenye ilichongwa na , mit einem Natursteindach von rund elf Metern Durchmesser und einem Meter Dicke, das aus einem einzigen, aus Istrien stammenden Monolithen herausgemeißelt wurde.
  • Kanisa la Ubatizo la Waariano (karne ya 6)
  • Kanisa la Ubatizo la Waorthodoksi (karne ya 5), nördlich des Doms, auch Neonische Taufkapelle genannt, gilt unter den achteckigen antiken Bauwerken Ravennas als das älteste.
  • Kanisa la askofu (karne ya 6)
  • Kanisa la Sant’Apollinare in Classe

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ravenna kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.