Liturujia ya Kimungu

Liturujia ya Kimungu ni adhimisho la ekaristi kwa jina linalotumiwa hasa na Waorthodoksi na Wakatoliki wa Mashariki wanaofuata madhehebu ya Kigiriki.
Baada ya liturujia ya maandalizi, ina sehemu kuu mbili: moja ambayo inaruhusu wakatekumeni kuhudhuria, ya pili ni kwa ajili ya waamini waliobatizwa tu.
Liturujia ya maandalizi
[hariri | hariri chanzo]
Inafanywa na padri na shemasi peke yao ikimaanisha maisha yaliyofichika ya Yesu kabla ya kuanza utume wake.
Wanaingia kanisani, wanaheshimu picha takatifu zilizomo na kuvaa nguo za ibada.
Kisha wanaandaa mkate na divai katika meza ya pembeni.
Hatimaye shemasi analifukizia ubani kanisa lote na kutoa kauli kwa padri ili ibada ianze.
Liturujia ya wakatekumeni
[hariri | hariri chanzo]


Sehemu hii ya hadhara inaleta hasa Neno la Mungu kutoka Biblia ya Kikristo.
Inaanza na baraka ya padri juu ya altare kwa kutumia kitabu cha Injili.
Zinafuata litania na antifona kadhaa.
Halafu padri anaingia rasmi katika patakatifu akishika Injili.
Baada ya wimbo wa Trisagio na wa Zaburi, inatangazwa sehemu ya Nyaraka za Mitume, halafu inaimbwa Aleluya na kusomwa sehemu ya Injili.
Inaweza kufuata hotuba.
Hatimaye kuna litania nyingine kadhaa.
Ndipo wakatekumeni wanaporuhusiwa kuondoka.
Liturujia ya waamini
[hariri | hariri chanzo]





Ndiyo adhimisho la ekaristi yenyewe kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Baada ya litania mbili na wimbo wa Kikerubi padri anaingiza katika patakatifu vipaji vya mkate na divai kwa maandamano.
Inafuata litania nyingine, halafu busu la amani, Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli na anafora mojawapo, ambayo ndiyo kiini cha liturujia ya Kimungu ambamo vipaji vinageuzwa kuwa Mwili na Damu ya Kristo.
Inafuata litania nyingine tena, halafu inasaliwa Sala ya Bwana.
Kisha kuinamia Ekaristi, inatangazwa kwamba Matakatifu hayo ni kwa ajili ya watakatifu.
Wakati wa kuimba, ekaristi inaandaliwa kwa ajili ya kuliwa.
Hapo waamini wanalishwa Ushirika mtakatifu, halafu kuna nyimbo na sala mbalimbali (hata hotuba kama haijatolewa baada ya masomo) kabla ya kuruhusiwa kuondoka.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Eastern Rites: A family tree Ilihifadhiwa 12 Agosti 2020 kwenye Wayback Machine.
- The Divine Liturgies Music Project Ilihifadhiwa 19 Agosti 2006 kwenye Wayback Machine. Byzantine music in English for the Liturgies of St. John, St. Basil, St. James and the Presanctified
- The Divine Liturgy Ilihifadhiwa 7 Aprili 2008 kwenye Wayback Machine. Text with Bible References and line-by-line Greek to English translations
- The Divine Liturgy of the Russian Orthodox Church Ilihifadhiwa 15 Januari 2007 kwenye Wayback Machine. in English/Church Slavonic, including music (midi, mp3)
- Photos of Divine Liturgy Ilihifadhiwa 13 Februari 2007 kwenye Wayback Machine. from Russia
- The Divine Liturgy of St. John Chrysostomus of the Greek Eastern Orthodox Church - In Hellenistic New Testament Greek (Koine) and Modern Demotic Greek
Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki
- The Divine Liturgy of the Syriac Orthodox Church
- Download Coptic/Arabic Holy Liturgies in mp3 format from St-Takla.org
- Coptic Liturgy of St. BasilIlihifadhiwa 5 Machi 2012 kwenye Wayback Machine. Full text with explanations and commentary
- Coptic Liturgy of St. MarkIlihifadhiwa 5 Februari 2012 kwenye Wayback Machine. (also known as the Liturgy of St. Cyril) Full text
- Coptic Liturgy of St. GregoryIlihifadhiwa 24 Mei 2012 kwenye Wayback Machine. Full text with footnotes
- Ethiopian Divine Liturgy Ilihifadhiwa 4 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.
- Armenian Divine
- The Divine Liturgy of the Melkite Greek Catholic Church Ilihifadhiwa 5 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
- The Beauty and Wisdom of the Armenian Divine Liturgy Ilihifadhiwa 17 Machi 2008 kwenye Wayback Machine.
- "In Remembrance of the Lord Ilihifadhiwa 20 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
- Arak29 Badarak (Armenian Divine Liturgy) Ilihifadhiwa 2 Aprili 2012 kwenye Wayback Machine.
- Armenian Badarak Ilihifadhiwa 5 Januari 2008 kwenye Wayback Machine. Commentary
- Analysis of the Armenian Divine Liturgy Abp. Tiran Nersoyan
| Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Kimungu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
