Ijumaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ijumaa ni siku ya sita katika juma (wiki) ya siku saba yenye asili ya kiyahudi-kikristo. Iko kati ya siku za Alhamisi na Jumamosi. Katika hesabu ya kimataifa ya ISO 8601 ni siku ya tano.

Nchi kadhaa za Waislamu wengi zimeanza kutumia Ijumaa kama siku ya mapumziko kwa wafanyakazi na sehemu ya wikendi.

Siku ya tano au siku ya sita?[hariri | hariri chanzo]

Katika muundo wa juma wa kibiblia Ijumaa ni siku ya sita. Kanuni ya ISO 8601 ilibadilisha hesabu ya juma kufuatana na kawaida ya mapumziko ya "wikendi" kwenye siku za Jumamosi/Jumapili. Katika muundo huu Jumatatu hutazamiwa kama siku ya kwanza katika juma ya kazi hivyo inahesabiwa kama siku namba "1" ya wiki katika kalenda hata kama jumuiya za kidini zinasisitiza hesabu ya kibiblia na kawaida katika tamaduni nyingi inaendelea hesabu ya kale.

Jina la siku kwa Kiswahili na kwa lugha mbalimbali[hariri | hariri chanzo]

Katika lugha ya Kiswahili jina la siku halina namba ndani yake. Inaitwa kufuatana na lugha ya Kiarabu na utamaduni wa Kiislamu "ijumaa" kutoka neno la Kiarabu الجمعة al-juma'a yaani siku ya "jumuiya" ya Waislamu kukutana pamoja kwa sala kuu ya Ijumaa mchana. Pamoja na Alhamisi ni siku ya pekee ya juma yenye jina la Kiarabu.

Majina ya siku zingine yameanzishwa upya katika Kiswahili kuanzia Ijumaa kuzitaja kama Juma-mosi, Juma-pili n.k.

Lugha nyingi za nchi za Waislamu zafuata kawaida ileile zikitumia neno hili la Kiarabu kwa mfano kwa mfano Kiindonesia ni "Jumat" au Kitartari ambayo ni lugha ya Kiturki ni "Comğa" na kwa Kiuzbekistan ni Жұма (juma).

Katika lugha nyingi za Ulaya jina la siku hutunza kumbukumbu ya miungu iliyoabudiwa zamani za dini za Kiroma au Kigermanik kama vile Kifaransa "Vendredi" (siku ya Veneri /Venus) au Kiingereza "Friday" (siku ya Freya).

Siku za juma (wiki)
Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano - Alhamisi - Ijumaa - Jumamosi
Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ijumaa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.