Lugha za Kiturki
Mandhari
(Elekezwa kutoka Lugha ya Kiturki)
Lugha za Kiturki ni kundi la lugha zaidi ya 30 zinazozungumzwa kutoka Ulaya ya Mashariki hadi Asia ya Kati na watu milioni 210. Zinahesabiwa kuwa sehemu za lugha za Kialtai pamoja na Kichina, Kimongolia, Kijapani na Kikorea. Wasemaji wa lugha za Kiturki husikizana kwa kiasi kikubwa. Lugha ya Kiturki inayojulikana zaidi kimataifa pia yenye wasemaji wengi ni Kituruki cha Uturuki.
Asili ya wasemaji wa lugha za Kiturki inadhaniwa kuwa sehemu za Mongolia. Kati ya karne za 6 hadi 10 walisambaa hadi Asia ya Magharibi na baada ya kutwaa Milki ya Bizanti waliingia pia katika Ulaya ya kusini-mashariki.
Lugha za Kiturki zenye wasemaji wengi
[hariri | hariri chanzo]Lugha tatu kubwa za kundi hili ni
[hariri | hariri chanzo]- Kituruki wasemaji milioni 60 katika Uturuki na vikundi vidogo katika nchi za Balkani; kutokana na uhamiaji pia katika nchi za Ulaya ya Kati na ya Magharibi (Ujerumani, Uholanzi)
- Kiazeri (Aseri) wasemaji milioni 30 katika Azerbaijan na magharibi ya Uajemi
- Kiuzbeki wasemaji milioni 24 katika Uzbekistan, kaskazini ya Afghanistan, Tajikistan na magharibi ya China
Lugha za Kiturki zenye wasemaji zaidi ya milioni moja:
[hariri | hariri chanzo]- Kikazakhi wasemaji milioni 11 nchini Kazakhstan, Uzbekistan, China, Urusi
- Kiuiguri wasemaji milioni 8 hasa katika Shinjiang (China ya Magharibi)
- Kiturkmeni wasemaji milioni 6.8 Mio katika Turkmenistan na kaskazini ya Uajemi
- Kikirgizi wasemaji milioni 3.7 Kyrgystan, Kazakhstan, China ya Magharibi
- Kitshuwashi wasemaji milioni 1.8 katika Urusi (sehemu ya kiulaya)
- Kibashkiri wasemaji milioni 2.2 katika Bashkiria jamhuri ya shirikisho la Urusi
- Kitartari wasemaji milioni 1.6 kati ya Urusi ya kati hadi Sibiria
- Kikashgai wasemaji milioni 1,5 Mio Sprecher katika majimbo ya Uajemi ya Fars na Khuzistan
Mifano ya maneno ya lugha za Kiturki
[hariri | hariri chanzo]Mifano ifuatayo inaonyesha jinsi gani lugha za Kiturki zinavyofanana:
Kiswahili | Kiturki cha Kale |
Kituruki | Kiturkmeni | Kitatari | Kikazakhstan | Kiuzbeki | Kiuiguri |
---|---|---|---|---|---|---|---|
Mama | ana | anne/ana | ene | ana | ana | ona | ana |
pua | burun | burun | burun | boryn | murın | burun | burun |
mkono | qol | kol | qol | kul | qol | qo'l | kol |
barabara | jol | yol | ýol | jul | zhol | yo'l | yol |
mnene | semiz | semiz | semiz | simyz | semiz | semiz | semiz |
ardhi | topraq | toprak | topraq | tufrak | topıraq | tuproq | tupraq |
damu | qan | kan | gan | kan | qan | qon | qan |
majivu | kül | kül | kül | köl | kül | kul | kül |
maji | suv | su | suw | syw | suw | suv | su |
nyeupe | aq | ak | ak | ak | aq | oq | aq |
nyeusi | qara | kara | gara | kara | qara | qora | qara |
nyekundu | qyzyl | kızıl | qyzyl | kyzyl | qızıl | qizil | qizil |
anga | kök | gök | gök | kük | kök | ko'k | kök |