Nenda kwa yaliyomo

Patriarki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bartolomeo wa Konstantinopoli, Patriarki wa kiekumeni.

Patriarki (kutoka Kigiriki πατήρ ἄρχων patèr àrchon, yaani "baba-kiongozi") ni cheo cha juu kati ya maaskofu wa Makanisa ya Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na wa mapokeo ya Mashariki ya Kanisa Katoliki.

Chini yake wako maaskofu wakuu na maaskofu wote wa mapokeo fulani au wa nchi fulani pamoja na waamini wao.

Kati ya mapatriarki wote wa Mashariki, muhimu zaidi kimapokeo ni yule wa Konstantinopoli, kwa kuwa mitaguso ya kiekumene ya karne ya 4 iliorodhesha maaskofu muhimu zaidi ya Kanisa kuanzia yule wa Roma, halafu Konstantinopoli, Aleksandria, Antiokia na Yerusalemu.

Hata hivyo Patriarki wa Moscow na wa Urusi wote ndiye mwenye waamini wengi zaidi.

Kumbe katika Kanisa la Kilatini cheo cha Patriarki hakileti mamlaka yoyote ya pekee.