Hidrati kabonia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Hidrati kabonia (pia: kabohidrati au hamirojo) ni kampaundi ya kikemia inayojengwa kwa oksijeni, hidrojeni na kaboni. Katika kemia huitwa kwa jumla kwa jina "sukari" hata kama sukari kwa lugha ya kawaida ni sehemu ya hidrati kabonia tu.

Hidrati kabonia ni kati ya molekuli muhimu zinazojenga viumbehai na mimea duniani. Kazi zao ni nyingi kwwa mfano kuhifadhi na kubeba nishati (wanga) ndani ya mwili wa wanyama na mimea au kujenga mwili kwa umbo la selulosi au chitini cha wadudu.

Umbo la kimsingi wa hidrati kabonia ni monosakaridi (Cn(H2O)n) zinazoungana kuwa aina nyingine za kabohidrati.

Aina za hidrati kabonia ni kwa mfano:

Chakula[hariri | hariri chanzo]

Hidrati kabonia ni chanzo cha nishati katika chakula cha watu wengi. Takriban asilimia 40 - 75 za mahitaji ya nishati ya watu hutokeana na hidrati kabonia. Vyakula vyenye hidrati kabonia nyingi ni vile vyenye wanga hasa nafaka na vyote vilivyotengenezwa kwa kutumia nafaka kama vile ugali, mkate, pasta, wali pamoja na mazao kama viazi na ndizi.

Katika utamaduni chache watu hula kabohidrati kidogo na karibu chakula chote ni protini ya kinyama kama vile kati ya Eskimo au Massai wanaokula hasa protini lakini mwili unaweza kubadilisha protini kuwa kabohidrati isipokuwa lishe yake inapungua.


Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hidrati kabonia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Chem template.svg Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hidrati kabonia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.