Kisukari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kisukari au bolisukari (jina la kitaalamu: diabetes mellitus) ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya glukosi katika damu. Sababu yake ni uhaba wa homoni ya insulini mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili wa kukubali insulini.

Dalili za kisukari ni

  • kukojoa kupitia kiasi cha kawaida
  • kiuu kikubwa
  • kuona vibaya na matatizo ya macho hadi kuwa kipofu
  • kuchoka haraka
  • vidonda vinavyopoa polepole mno hasa kwenye miguu hadi kupotea viungo

Watu wachache huzaliwa na uhaba wa insulini. Watu walio wengi wana ushaifu fulani unaokuwa hatari kutokana na aina za vyakula na maisha ya kila siku. Kutumia sukari nyingi pamoja mafuta mengi katika chakula na vyinywaji, kukosa mazoezi ya mwili (kwa watu wenye kazi ofisini), kunywa pombe nyingi na kuvuta sigara huongeza hatari ya kushika kisukari kuanzia baada ya miaka ya ujana.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]