Sudan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
جمهورية السودان
Jumhuriyat as-Sudan

Republic of the Sudan
Bendera ya Sudan Nembo ya Sudan
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Al-Nasr Lana (Kiarabu: Ushindi ni Wetu)
Wimbo wa taifa: نحن جند للہ جند الوطن Nahnu Jund Allah Jund Al-watan ("Sisi ni Jeshi ya Mungu na Nchi yetu")
Lokeshen ya Sudan
Mji mkuu Khartoum
15°00′ N 30°00′ E
Mji mkubwa nchini Omdurman
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali
Rais

Omar al-Bashir
Uhuru
 - Tarehe
Kutoka Misri na Uingereza
1 Januari 1956
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,886,068 km² (ya 16)
5%
Idadi ya watu
 - Julai 2006 kadirio
 - 1993 sensa
 - Msongamano wa watu
 
36,992,490 (ya 40)
31,894,000
16.4/km² (195)
Fedha Dinar (SDD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
MSK (UTC+3)
not observed (UTC+3)
Intaneti TLD .sd
Kodi ya simu +249

-


Ramani ya Sudan ikionyesha majimbo yake

Jamhuri ya Sudan, ama Sudan ni nchi kubwa ya tatu ya Afrika kulingana na eneo.

Imepakana na Misri kaskazini, Bahari ya Shamu kaskazini-mashariki, Eritrea na Ethiopia mashariki, Sudan Kusini kusini-mashariki, Afrika ya Kati na Chadi magharibi, na Libya kaskazini-magharibi.

Kijiografia nchi hii huhesabiwa kama sehemu ya Afrika ya Kaskazini.

Mji mkuu ni Khartoum.

Majimbo ya Sudan Kusini yalikuwa sehemu ya nchi hiyo lakini yalipiga kura ya kujitenga yakapata kuwa nchi huru kuanzia tarehe 9 Julai 2011.

Sanamu ya Mfalme wa Wanubi, Sudan
Aliyekuwa makamu wa Rais John Garang, ambaye aliongoza wanamgambo wa Sudan ya Kusini kupigania uhuru wa majimbo ya kusini.

Maeneo ya Sudan[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya siasa ya Sudan kabla ya Sudan Kusini kujitenga.

Majimbo[hariri | hariri chanzo]

Madaraka, Kujigawa, na Vita[hariri | hariri chanzo]

Makabila ya kusini yalipigania vita ndefu hadi kupata uhuru.

Darfur ni eneo yenye majimbo matatu ambaye imeathiriwa na vita vya kisiasa, vita vya Darfur.

Pia kuna wanamgambo upande wa mashariki Umbele wa Mashariki.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mlima wa Dair eneo ya kati, Sudan
bwawa kusini Sudan

Sudan iko upande wa Afrika ya kaskazini, imepakana na bahari ya Shamu kati ya Misri na Eritrea. Imetamalikiwa zaidi na mto Nile na mikono yake.

Kwa eneo ya kilomita mraba 1,886,068 (728,215 sq mi), ni nchi ya tatu kwa ukubwa katika bara la Afrika na ya kumi na sita duniani.

Ardhi yenyewe ni kiwara, lakini kuna milima upande wa mashariki na magharibi.

Hali ya anga ni ya mwangaza kusini, na mikuranga kaskazini. Mvua yapatikana mwezi wa Aprili na Oktoba. Kudhoofika kwa mazingira hasa ni kwa sababu ya mmomonyoko wa udongo na utapakazi wa jangwa.

Ona pia: Orodha ya miji Sudan

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Watu na makabila[hariri | hariri chanzo]

Kadiri ya sensa za mwaka 1993, wakazi walihesabiwa kuwa milioni 26. Hakuna sensa nyingine iliyofanywa kutoka mwaka huo kwa sababu ya Vita vya wenyewe kwa wenyewe. Umma hasa wakadiriwa na kitabu cha wadadisi wa Marekani kuwa milioni 39 mwaka 2004.

Umma wa miji kama Khartoum (na pia Khartoum, Omdurman, na Khartoum ya kaskazini) waongezeka zaidi, umma wa miji hii yakadiriwa milioni 6-7 na wengine wahamiaji milioni 2 ambao wamekimbia vita vya kusini, magharibi, mashariki na pia wengine kwa sababu ya ukame.

Sudan ina aina mbili za utamaduni — Waafrika walio na Uarabu na Waafrika wasio Waarabu — na maelfu ya makabila na migao ya kabila, lugha tofautitofauti kwa makundi au kabila – migawanyiko hii uleta siasa za utengo na ubaguzi.

Majimbo ya Kaskazini hasa ndio makubwa nchini Sudan, na pia miji mikubwa iko katika majimbo haya. Zaidi ya milioni 22 wanaoishi katika majimbo haya ni Waislamu-Waarabu na wanaongea Kiarabu, lakini wengi pia huongea lugha za kikabila hasa Kinubi, Kibeja, Kifur, Kinuban, Kiingessana, kwa kikundi hiki kuna wale wavutia zaidi kama: Wa-Kababish kutoka kaskazini Kordofan, watu hawa wanaofuga ngamia; Ga’alin (الجعلين), Rubatab (الرباطاب), Manasir (المناصير) and Shaiqiyah (الشايقيّة); makabila ambao kikao chao ni karibu na mito ni kama Baggara wa Kurdufan na Darfur; Wakiham Beja eneo ya bahari ya Shamu na Wanubi wa kaskazini Nile, ambao wengine wamehamishwa karibu na mto Atbara. Eneo la Shokrya kwa Wa-butana, Wa-bataheen wamepakana na Waga’alin na Washorya, upande wa kusini-magharibi eneo ya Butana. Pia kuna Warufaa, Wahalaween na makabila mengine mingi eneo la Gazeera na kwa ufuo wa Bluu Nile na eneo ya Dindir. Hata Wanubi kusini mwa eneo la Kurdufan na Wafur upande wa magharibi.

Watu wa Sudan[hariri | hariri chanzo]

(zaidi, eneo ambazo zimechapika)

  • Nyingine zaidi

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Dini[hariri | hariri chanzo]

Dini kubwa zaidi ni Uislamu (97%).

Wakristo ni waumini hasa wa Kanisa Katoliki, Anglikana Kanisa ya Sudan, Wapresbiteriani na Wakopti wa Sudan.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Vyuo Vikuu vya Sudan:

Ona pia[hariri | hariri chanzo]

Vifungu Kiwazowazo[hariri | hariri chanzo]

Viungo via Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Maarifa ya Kawaida

<!—Tafadhali usiweke maadishi au kifungu kuhusu biashara hapa, kwa mfano; vitabu vya Sudan --> <!—Ukiweka maadishi hayo, waweza KUFUNGIWA kuhariri Wikipedia! -->

Serikali

Habari

Picha

(Sura mpay ya sudan)

Utalii

Nyingine


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia