Gamal Abdel Nasser

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gamal Abdel Nasser

Gamal Abdel Nasser (kwa Kiarabu جمال عبد الناصر ‎gamal abd-an-nasir); (Alexandria, 15 Januari 1918; Kairo, 28 Septemba 1970) alikuwa mwanajeshi na rais wa Misri katika miaka 1954 hadi 1970.

Alikuwa kati ya viongozi wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1952 nchini Misri iliyompindua mfalme na kuanzisha jamhuri.

Mwaka 1956 alitaifisha mfereji wa Suez uliokuwa mali ya kampuni ya kigeni akaamuru kujengwa kwa lambo la Aswan tangu 1958.

Alijenga jeshi kubwa lililoshindwa mara mbili katika vita dhidi ya Israel.

Katika siasa ya ndani alijaribu kupeleka Misri mbele kwa kuwapa wakina mama haki ya kupiga kura katika uchaguzi na elimu bila malipo kwa vijana wote. Wakulima wadogo walipewa mashamba.

Lakini utawala wa serikali katika sehemu nyingi za uchumi uligonga ukuta kama katika nchi mbalimbali yaliyofuata utaratibu wa uchumi wa kupangwa na serikali.

Nasser alihesabiwa kati ya mashujaa wa harakati ya nchi zisizofungamana na upande wowote katika vita baridi kati ya Umoja wa Kisovyeti na Marekani.

Mwaka 1967 maazimio yake yalikuwa kati ya sababu za vita ya siku sita kati ya Israel na majirani Waarabu.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gamal Abdel Nasser kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.